Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,086
- 1,081
Msumbiji wameanza kuzalisha kinywaji cha Impala beer kwa kutumia mihogo. Hadi sasa Impala ndicho kinywaji kinacho pendwa na wananchi wengi kwani watu wenye kipato cha chini wanamudu bei yake, na kwa sasa Impala inashika nafasi ya tatu kwa idadi ya wateja.
Kilimo cha mihogo kwa sasa kimeingia kwenye kundi la kilimo cha biashara na wananchi wengi wameingia kwenye kilimo cha mihogo kwani soko la uhakika lipo.