In A Box Innovations: Washauri wa Masuala ya Radio Waliobobea.

In A Box Innovations: Washauri wa Masuala ya Radio Waliobobea.

Radio Producer

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2011
Posts
726
Reaction score
320
Wadau,

huduma zetu hizi hapa:-

1. vifaa vya radio vya aina mbalimbali tunauza.
2. Ufundi wa vifaa vya radio.
3. ushauri wa kitalaamu juu ya kuanzisha radio.
4. Kusimamia mwanzo hadi mwisho uanzishwaji wa radio yako mpaka masuala ya TCRA.
5. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wako.
6. Kuboresha radio yenu kama huwa haina wasikilizaji ikaongeza wasikilizaji.
7. Aisee mambo ni mengi unaweza tu kuwasiliana nasi hapa: consultancyradio@gmail.com
 
Safi sana nilitaka kujua gharama maana sijui sana nafikiri ni watu wenye Mipesa mingi ndio wenye ubavu,
Vipi kama tuna Million 25 za Kitanzania tunaweza kuwa hewani na kwa Umbali gani????
 
Safi sana nilitaka kujua gharama maana sijui sana nafikiri ni watu wenye Mipesa mingi ndio wenye ubavu,
Vipi kama tuna Million 25 za Kitanzania tunaweza kuwa hewani na kwa Umbali gani????

Kwa hiyo pesa unaweza kuwa hewani kwa Km 45 za maraba ground level na ukifungiwa vizuri unaweza kufika mpaka 60KM Asante na karibu sana.
 
Kwa hiyo pesa unaweza kuwa hewani kwa Km 45 za maraba ground level na ukifungiwa vizuri unaweza kufika mpaka 60KM Asante na karibu sana.
1. Unaposema GROUND-LEVEL una maana gani?????
2. Kama nikifunga radio ya M 25 baadaye nikapata zingine naweza kui-UPGRADE ikawa bora zaidi???
3. Ni kitu gani kinachowezesha radio irushe matangazo mbali ni ANTENA au TRANSMITER???
4.Kama uwezo wangu ni mdogo je naweza kununua vitu leja-leja wakati niko hewani???????
 
Mpendwa ndugu mwana JF yafuatayo ni majibu yako:-
1. Tunaposema ground level tunamaanisha ni mawimbi yanayosikika usawa wa ardhi yaani ni sehemu ambako radio yako itapatikana bila kuitafuta tafuta.
2. Ndiyo radio huwa unapanuliwa. Mfano kama umeanza na transmitter ya watts 300 unaweza kuja kubadili ukaweka ya watts 1000 au 1500 na baadae unaweza ukapanua hata kwa kuweka booster. Kama upo Kilimanjaro na unasikika mpaka Arusha unaweza kuweka booster Arusha ukasikika mpaka Babati, Kateshi n.k ni mfano tu.

3. Inategemea na system unatotumia, kama una mnara basi utahitaji antenna, Transmitter na STL (yaani Studio Transmitter Link)

4. Kununua vitu reja reja inawezekana cha msingi kwa mara ya kwanza ukamilishe vyakuanzia.

thanks and welcome
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri hasa jibu lako namba 4 ni vitu gani vya kuanzia na vina gharama gani maana nataka kujitosa mda si mrefu
 
Back
Top Bottom