Kauli mbiu ya CCM Zanzibar ni; "mapinduzi daima" na serikali ya Zanzibar inajulikana kama serikali ya mapinduzi! Na rais wake pia ni Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi. Katika hali hiyo utakubaliana nami ya kuwa serikali iliyowekwa na wananchi kwa kura, haiwezi kuitwa serikali ya mapinduzi. Ikumbukwe, marehemu Karume aliwahi kusema ya kuwa, madaraka yaliyopatikana kwa mtutu wa bunduki, huwezi kuyapoteza kwa makaratasi; akiwa na maana ya kura. Kwa kujua hilo, inaelekea maalimu Seif aliona vema akampisha mwana haramu apite.