Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Jamani hivi mmegundua kuwa tangu itangazwe kuwa kuna upungufu wa Maji unaosababisha mgawo, DAWASA wameanza kuzibua Visima 161 mitaani huko ambavyo havikuwa vikifanya kazi.
Kwa jinsi hali ilivyo ni wazi kabisa kuwa hawa jamaa DAWASA hawana kawaida ya kuchukua tahadhari yoyote kuhusu dharula ya Maji hasa kwa nyakati za kiangazi au hali yoyote itakayojitokeza hasa kwa jiji la Dar es salaam.
Nadhani imefika wakati sasa Serikali ifikirie kutoa nafasi kwa sekta binafsi ziendeshe miradi yenye mahitaji muhimu ikiwemo umeme na maji ili kuleta ushindani kwenye huduma lakini iweke sheria za udhibiti wa bei na ubora.
Maana kwa hal hii tunaenda kubaya sana huko mbele, wiki ya pili mitaani hakuna maji na viongozi bado wako ofisini, uwajibikaji uko wapi sasa jamani?