“…watu wanauawa hovyo huko…waambieni wanasiasa kwamba vyeo havipatikani kwa kuua watu, kwa kunyofoa viungo…” – Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuguswa na wimbi la utekaji na mauaji ya watoto linalodaiwa kuendelea maeneo mbalimbali hapa nchini…akiwaomba machifu kote nchini kusimama imara na kuilinda jamii kwa kuonya na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.