Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Inasikitisha sana tena inahuzunisha kuona ripoti ya CAG ya safari hii baada ya mwendazake kuzikwa, ikiibua madudu mengi mno, tofauti na ripoti zilizokuwa zikiwakilishwa hapo nyuma wakati wa utawala huu wa awamu ya 5 ambazo zilikuwa zinampamba sana mwendazake na kueleza Taifa letu linapaa sana kiuchumi!
Ushahidi wa mazingira ya ninachokisema hapa ni kutokana na kauli aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akipokea ripoti hiyo akimwelekeza CAG kicheere kuwa hapaswi kuwa na kigugumizi chochote na anapaswa kueleza kila kitu kwa uwazi katika ripoti yake ili watanzania ambao ndiyo walipa kodi wa nchi hii, waelewe namna pesa yao inavyotumika.
Nasema kuwa ripoti za awali zilikuwa zinakuwa "edited" kwa kuwa katika ripoti za nyuma za CAG tulikuwa tukiambiwa kuwa ATCL imetengeneza faida ya Shilingi bilioni 28, wakati katika ripoti hii ya CAG inasema wazi kuwa katika miaka 5 ya nyuma mfululizo, ATCL imekuwa ikipata hasara na katika mwaka Wa fedha wa 2019/2020 ilipata hasara ya shilingi bilioni 60!
Vile vile tujikumbishe kile kilichompata CAG aliyepita, Profesa Mussa Assad baada ya kuibua ufisadi wa shilingi trillion 1.5 nini kilimpata baada ya kuibua ufisadi huo?
Kila mwananchi wa nchi hii ni shahidi namna CAG huyo alivyoundiwa "zengwe" na Spika Ndugai na Mwendazake, kwa kudhalilishwa sana hadi akatishiwa na Spika Ndugai kuwa akigoma kuja kuhojiwa na Kamati yake ya maadili, basi ataviagiza vyombo "vyake" vya dola vimlete pale bungeni akiwa amefungwa pingu mikononi!
Nini kilimpata CAG huyo kila mwananchi ni shahidi, namna CAG huyo alivyofurushwa kwa nguvu na kutimuliwa kazi!
Hivi kwa hii "trend" inayoendelea hapa nchini, ni mwananchi gani atakayeamini takwimu zilizokuwa zonatolewa chini ya utawala wa mwendazake, ambazo kwa maoni ya wananchi walio wengi zilikuwa ni za kughushi na zilizojaa uzushi na propaganda nyingi?