Mkuu sijakuelewa? Una maana gani? Wewe unachanganya kati ya wakandarasi na Wahandisi. Mtu yoyote anaweza kuwa Mkandarasi ili mradi tu awe na Caapital. Uhandisi unapatikana kwa kusoma. Unajuaje kama kwenye hiyo kampuni ya Kichina hakuna wahandsi wa kibongo? Mkuu hao consultants waliopo hapo sio wabongo? Nazungumzia Structural Engineer, Service Engineer, Architect na Quantity Surveyor.
Mkuu hujui labda huo mradi unajengwa kwa niaba ya Watu wa China, unategemea atapewa mbongo?Miradi mingi ikijengwa kwa niaba ya Watu wa nchi nyingine, huwa wanakuja na kambuni zao.
Kumbuka kuna daraja litaanza jengwa kama sijakosea litakuwa Igunga, Wakandarasi wa Kibongo wamejiunga na kupewamradi huo. Hapa najiuliza wametumia vigezo gani, walishinda tenda?