Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,258
- 10,014
Kwanini Yanga walilazimisha kwenda uwanjani hata baada ya mechi kuahirishwa hiyo tarehe 8 Machi 2025?
Ilikuwa ni kwenda kuondoka na majini na uchawi wao waliouacha uwanjani. Hakukuwa na namna nyingine ya kuhamisha uchawi wao mara baada ya bodi ya ligi kutangaza mechi haipo. Sasa wanaingiaje uwanjani? Ilikuwa ni lazima wajitoe ufahamu, wadai hawatambui mechi kuahirishwa na wanaenda uwanjani. Ni kweli walienda na wakafanikiwa kuingia na kufanya yao.
Majini yao waliyaaminisha ni lazima yatakutana na Simba. Yakaendelea kudai kukutana na Simba ikabidi ili kuyaridhisha wapaleke Bunju Mo Arena yakutane na Simba.
We fikiria tu kwa akili ya kawaida. Inawezekana vipi mtu awashe gari tena basi kubwa namna ile kuelekea Bunju kisa kucheza na Simba Mo Arena baada ya jana yake mechi kuahirishwa. Watu wanaweza kuona ni kama utani utani vile lakini tunaooona mbali tunajua ni nini wanafanya. Au nasema uongo ndugu yangu Mshana Jr Scars OKW BOBAN SUNZU na wengineo