Inabidi itumike akili gani kuwaelezea watanzania kwamba vita ya Ukraine na Russia sio ya kuishabikia?

McCollum

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2023
Posts
384
Reaction score
684
Habari kwa wanajamvi!

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada, kwa watanzania wengi (nitasema wengi licha ya kwamba sijafanya utafiti ila naona kwa ninachokumbana nacho mtaani inawezekana wengi wana mawazo hayo hayo) wanaivalia njuga vita inayoendelea baina ya mataifa mawili ambayo kiasili yalikuwa taifa moja ambayo ni Ukraine na Urusi. Vita hivi vimezalisha nyuzi nhingi na baadhi ya watu wamejimega na kujiweka kwenye upande wa Ki-Russia na wengine wanakimbilia Ukraine.

Shida hapa sio unazi ila shida ipo kwenye kuamini kwamba madhara ya vita hivi yanaishia huko huko Ukraine na Russia na hivyo huku Tanzania wazee kwa vijana wanabaki wakipiga stori za ajabu ajabu wakidai kwamba Russia ana bomu kubwa akipiga dunia nzima inapotea and the like?

Kwa unavyodhani itumike akili gani kuwabadili mawazo hawa wanaojiita Warusi wa kwa mtogole na wa Ukraine wa Tegeta (Majina ni kwa ajili ya fun tu 🤣🤣🤣😂 ila ni matumaini yangu thread imefikisha ujumbe muafaka)
 
Kwani kushabikia shingapi? 🙂
 
Ile kitu wanaita " European value" yani mambo ya ushoga na vitu ka hizo, sina huruma serikali na jeshi la Ukraine, sema wananchi wanateseka kwa faida ya wahuni wachache.

By the way, Bakhmut has fallen to Wegner 🇷🇺🇷🇺🇷🇺🇷🇺
 
Back
Top Bottom