Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 579
Mambo ya ndani na mwenza wako hayafai kuyasema kijiweni au nje. Udhaifu wa mwenzako unatakiwa kumsaidia muumalize ndani kwa ndani, kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu. Wewe unapowaambia wenzako mkeo habadilishi nguo ya ndani wiki nzima unataka wenzako wakuonee huruma gani? Kwa nini usimfunze kwa kuichukuwa ukamfulie halafu uone reaction yake? Au, umemnunulia nguo za ndani na ukaona bado habadilishi? Naye akikusema kwa wenzake kwamba unalala doro mtalimbo wako sekunde moja tu unadhani watakuonaje watu unapopita mtaani? Kumwambia nyumba ndogo kwamba mkeo "kama gogo" unamkosea mkeo sana na utalipia ufidhuli huo mpaka ukome, maana wakijua udhaifu wako watakuchomoa mpaka ushindwe kununua kanda mbili.
Kuna mambo ambayo mtu mzima hatarajiwi kuambiwa afanye, yeye mwenyewe kama anayo akili sawasawa anatarajiwa kupima na kuamua afanye nini. Kama mwenzako ni mdhaifu na ameshindwa kutatua udhaifu wake maana yake na wewe ni mdhaifu vivyo. Kama wewe ungekuwa zaidi ungemnasua aondokane na udhaifu wake. Kama mke anavyojisikia vizuri kusifiwa na mumewe, kadhalika mume anajisikia vizuri akisifiwa na mkewe.
Uking'ang'anizi wa mkao mmoja miaka nenda miaka rudi nyumbani kwenu ndio unaofanya vyumba vyenu vichuje kwa kasi na hata mkaanza kutazamana kama mazezeta. Kabla hamjaungana mlikuwa mko hyper hyper kila mtu kwa mwenziwe, sasa hamjiulizi inakuwaje chumvi haijakolea siku hizi ila kwa jirani tamu sana "chai" yake?
Dunia imebadilika sasa na mdudu anawakodolea watu awameze kila kukicha. Kila mtu akae kwenye nafasi yake na ndoa zetu zitakuwa tamu kila leo. Mkate wa kuiba ni mtamu lakini madhara yake ni makubwa.