A
Anonymous
Guest
Hospitali ya Massana ambayo ipo mitaa ya Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam ipo mbioni kufilisika au kufa kabisa kutokana na zoezi la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuchukua fedha kwenye Akaunti za Benki za Hospitali hiyo kwakile wanachodaiwa kuwa ni madeni wanayoidai Hospitali.
Kwasasa sisi Watumishi na Wafanyakazi wa Massana Hospitali hatujalipwa mishahara tangu Mwezi Mei 2024, hata miezi ya nyuma pia mishahara yetu ilikuwa ya kusuasua.
Mwanzoni mwa Mwaka huu (2024) viongozi wetu walitudokeza kuwa TRA imekuwa ikichukua fedha zote kwenye Akaunti za Hospitali hiyo kiasi kwamba ofisi yetu imeyumba.
Hali inatoendelea tayari uongozi wa Hospitali umetangaza hali ya tahadhari kwetu wote tunaotumikia ajira zetu katika taasisi hiyo ya afya.
Massana Hospitali inahudumia Wagonjwa lakini pia ina Chuo cha Afya na Wafanyakazi wote wa pande zote hatujapokea mishahara, mazingira ambayo yamesababisha huduma tunzotoa zianze kusuasua.
Niwe wazi kama ni kweli TRA wo ndio chanzo cha hiki tunachopitia, basi wao ndio chanzo cha Wafanyabiashara au watoa huduma wengi wetu kuwa na hali mbaya za kimaisha, tunakoselea TRA inaua taasisi yetu na inaelekea kutumaliza Watanzania zaidi ya 100 tunaotegemea Hospitali ya Massana kuendesha maisha yetu pamoja na wale ambao wanatutegemea.
Tunamuomba Waziri wa Afya huyu mpya aliyeingia madarakani kuja kuokoa ajira na maisha yetu kwani wengine tuna wategemezi wengi nyuma yetu, anguko la waajiriwa wa Massana ni anguko la mamia ya Watanzani wengine walio nyuma yetu.
Mbali na hapo sisi Watumishi wa afya tunahitaji kuwa na ukamilifu Kisaikolojia ili tutimize majukumu vizuri kwa kuwa tunahusika na afya za watu, kushughulikia fya ya mtu wakati wewe afya yako ya akili haipo sawa ni hatari.
Rais Samia Suluhu ujumbe huu ukufikie Watanzania wenzako tunateketea huku tunajiona, msaada wako unahitajika.