Inachukua siku ngapi wastani kutoa gari bandrini?

JipuKubwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
2,341
Reaction score
2,390
Heri ya mwaka mpya wana jamvi, nawatakia 2022 wenye baraka

Kwenye mada,naomba kuuliza inachukua muda gani kutoa gari bandarini baada ya meli kushusha, maana ni muda sasa tangu meli ishushe wakala hajanikabidhi gari yangu ilikuwa niitumie kwenda Rombo kusalimia wazee.Msaada tafadhali kwa wajuzi wa haya mambo.

Asante.
 
Mkuu, kama umeshalipa ushuru ni siku 1 tu hadi 2 zinatosha.

Hebu fuatilia usije ingia kwenye storage.

Je ushuru ulilipa wewe au ulimpa wakala akulipie?

Port charges, na tozo zingine umelipa wewe au wakala na lini?

Mwisho meli imeshusha lini?
Asante sana mkuu,ushuru kalipia wakala na meli ilishusha 19/12/2021...wakala aliniambia kwamba mwisho wa mwaka wafanyakazi wengi walienda kula sikukuu.
 
Asante sana mkuu,ushuru kalipia wakala na meli ilishusha 19/12/2021...wakala aliniambia kwamba mwisho wa mwaka wafanyakazi wengi walienda kula sikukuu.
Hapa ndo ulipokosea Mkuu, ulitakiwa ulipe mwenyewe kazi yake alitakiwa akupe control number za TRA na TBS.

Uliagiza kupitia kampuni gani?

Je, ulikuwa unafuatilia meli iliyokuwa imebeba gari yako?

Nina wasiwasi na wakala huyo mbona TRA, TPA, TASAC na TBS muda wote wako kazini kipindi hiki.
 

Mkuu huyo anashida kama yangu, mm nmeagiza kupitia meli ya Silver ray, ambapo ilifika tanzania 29/12/2021


Nami nmeagiza kupitia wakala, ila nmekua nikiifatilia meli tangu Japan.

Wakala kanambia kuprocess Clearing and Forward ni ndani ya siku 7.

Sijui ni sahihi?
 
Asante sana mkuu,ushuru kalipia wakala na meli ilishusha 19/12/2021...wakala aliniambia kwamba mwisho wa mwaka wafanyakazi wengi walienda kula sikukuu.
Huyu wakala ni muongo.

Bandari inafanya kazi 24x7x365


Muombe documents zote hapo ilipofikia.

Kama kalipa ushuru mwambie akuonyeshe evidence.

Pia ni wakala wa kuagiza gari au wakala wa forodha?

Wewe upo na documents gani zinazohusu gari?
 
Ndani ya siku 7 nikuwa hakuna storage charges ndani ya hizo siku 7.

Ila kama meli imeshusha gari inatoka ndani ya masaa 36 unakuwa nayo mkononi.

Umeshalipa ushuru?

Umeshalipia chochote kihusucho bandari?
 
Ndani ya siku 7 nikuwa hakuna storage charges ndani ya hizo siku 7.

Ila kama meli imeshusha gari inatoka ndani ya masaa 36 unakuwa nayo mkononi.

Umeshalipa ushuru?

Umeshalipia chochote kihusucho bandari?

Mkuu, Nami nliingia chaka nkamuachia wakala afanye kila kitu, yani pesa zoote nlimkabidhi wakala.....ila umenifungua macho, ngoja nianze kumfatilia na kujua kila hatua aliyofikia.
 
Nakubali hapa nimekosea,nimejifunza kitu...asante sana mkuu.Nimefuatailia meli toka Japan hadi Mombasa kisha Dar.Ngoja nikomae naye hadi kieleweke.
 
Mkuu mimi ni wakala wa forodha, ugomboaji wa gari bandarini huchukua siku 2 mpaka 3 mara baada ya meli kushusha.

Kesi yako Silver Ray ilimaliza kushusha usiku wa kuamkia jana tarehe 31/12/2021 hivyo kama kodi na TBS inspection fee umelipa kesho Jumapili au Jumatatu wakala ataigomboa gari yako

Kwa huduma za Clearing and Forwarding na ushauri wasiliana nami;

Ruaha Freight Ltd,
Samora Avenue,
7th Floor, Twiga Houuse,
Mob: +255718 866 651 ( whatsap/Call).

 

Shukrani sana mkuu[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Inatakiwa isizidi siku 7 baada ya hapo unaanza kulipia gharama ya utunzaji (storage).

Ila muda mwingine unaweza kukuta meli imefika imekuta kuna foleni ya meli zingine kushusha ikabidi isubiri ila mara nyingi kama isipokuta foleni inachukua siku 2 hadi 3 kama mdau alivyosema hapo juu.
 
Huyu wakala ni muongo.

Bandari inafanya kazi 24x7x365


Muombe documents zote hapo ilipofikia.

Kama kalipa ushuru mwambie akuonyeshe evidence.

Pia ni wakala wa kuagiza gari au wakala wa forodha?

Wewe upo na documents gani zinazohusu gari?
Nakubaliana na ww mkuu kazi haijawai kusimama kisa sikukuu nchi haiendi hivyo, kama aliagiza kupitia wabongo wengi wao ni waongo [Sisemi ni wote], utakuta ameshaipokea gari ila anaenda kuipiga polish na kushusha kilometa wengine hadi kung'oa vifaa vizuri na kuviuza.

Kuna uzi humu ulishawahi kuwekwa kuhusu janja janja ya waagizaji wa kibongo.
 
Kashapigwa tayari
 
Aandae na chai ya TBS si unajua tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…