Kuna abiria wanaosafiri kutoka Nyamisati kwenda Mafia wamekwama bandarini tangu Jumatatu hadi leo wakisubiri usafiri na hakuna sababu za msingi zinazotolewa, watu wanaambiwa wasubiri.
Sasa wasubiri hadi lini na mazingira ya kule ninyi mnayajua? Watu wana watoto wachanga kule, wahusika mko wapi kama kuna tatizo kwanini msiseme ili watu wakajua....
Mnatesa sana watu, mamlaka husika kama mpo humu taarifa ndio hii wapeni wananchi ufumbuzi maana wanateseka kule
=======================================
Taarifa rasmi kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupitia kwa Ofisa Habari, Alfred Mgweno ameeleza kuwa ni kweli Kivuko cha Mv. Kilindoni kimesimama huduma kwa muda kutokana na kuwa katika matengenezo ya mlango wa kivuko.
Akizungumza na JamiiForums amesema “MV Kilindoni ipo Mafia inafanyiwa matengenezo kidogo ya mlango na itaendelea na safari zake Jumamosi ya keshokutwa (Februari 19, 2022), kivuko kingine cha jeshi kipo Nyamisati kinasubiri mafuta ili kuendelea na safari zake,” - Mgweno.