Inadaiwa baadhi ya majeshi ya Urusi yaliyokuwa Belarusi kwa ajili ya mazoezi ya Kijeshi yaanza kurudi, baada ya mazoezi kuisha

Inadaiwa baadhi ya majeshi ya Urusi yaliyokuwa Belarusi kwa ajili ya mazoezi ya Kijeshi yaanza kurudi, baada ya mazoezi kuisha

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Urusi na mahodari Sana wa mchezo unaotumia akila Sana wa CHESS. Wamefanikiwa kuzima propaganda za west kuwa Urusi ingeweza kuivamia Ukraine ndani ya mda mfupi Sana.

Urusi tayari imefanikiwa kupeleka ujumbe kwa west kwamba kwa ajili ya kulinda usalama wake iko tayari kwa lolote like,kuharibu uchumi wake na hata kuingia vitani na nchi yoyote,au umoja wowote,au hata kuivamia nchi yoyote itakayo kuwa mwenyeji wa maadui zake.

Na kwa nchi zinazojua umuhimu wa ulinzi wa mipaka na usalama wa Taifa lao,hua haiangalii Nini kitatokea Bali huangali ulinzi na usalama wa nchi. Ujumbe umefika bana.

Urusi imefanikiwa kuizuia Ukraine kujiunga na NATO.
Ukraine haitakaa kamwe iwaze Tena kusudio la kutaka kujiunga na NATO.
Ujumbe umefika.

Kwenye suala la kulinda mipaka na usalama wake Urusi imeonesha iko tayari kupambana na yoyote awe mmoja au wengi kwa pamoja,Yuko tayari kukabiliana nao.

Urusi aliwahi kuivamia Afghanistan akaikalia kwa miaka kumi. Nchi zilizokwenda kusaidia Afghanistan ili kumtoa Urusi ni Marekani na NATO,China, Pakistan,Saudi Arabia akiwasapoti kiuchumi akia Bin Laden na vitaifa vingine vidogovidogo.Lakini Mwamba alikaa miaka Kumi Hadi alipoamua kuondoa majeshi yake yaliyokuwepo Afghanistan na sehemu nyingine duniani baada ya kuona gharama ni kubwa mno za kuyahudimia majeshi.

Waliamua kuondoa majeshi ya yaliyokua yamewekwa sehemu mbalimbali duniani baada ya kuja na moango wao was mageuzi ya kiuchumi na kisiasa yaani "Perestroika na Glasnost". Hivyo Kama Ukraine angeshupaza shingo juu ya kuwakaribisha NATO hali ingekua mbaya zaidi ya Afghanistan.

Ukraine inatia huruma kwa kutaka kumkaribisha adui kwani hoja iliyopo katika bunge la Urusi ni kuyatambua majimbo ya Ukraine yaliyojitenga ya Donesk na Luhansk. Urusi ikiyatambua haya itakua ni aina nyingine ya Crimea crisis.

Urusi inatisha bana
Iliyatambua majimbo ya ossetia na Abkhazia huko Georgia baada ya Georgia kutunishiana misuli na Urusi. Na baada ya Urusi kutumia siku Chache Sana kuiadhibu Georgia.

Kama Ukraine itaruhusu maadui wa Urusi waingie Kiev basi tutegemee Ukraine kubakia Kama kuku aliekatwa mabawa,kwani majimbo ya Luhansk, Donesk na Donbass yatanyofolewa kutoka Ukraine.

Hakuna hata nchi moja ya NATO itaingilia Kijeshi kwa sababu nchi yoyote ya Ulaya Mwanachama was NATO kuingia vitani na Urusi ni kukubali kupoteazwa katika ramani ya dunia,ni kujitoa mhanga.

Je, Kuna nchi ulaya iko tayari kupoteazwa kwa sababu ya Ukraine?

Vita ya NATO na Urusi ni Vita ya tatu ya Dunia.
Je Ukraine ndo iwe chanzo?

Urusi wameshacheza karata zao vizuri Sana,Ukraine haiingii NATO Tena.
 
Vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vimeshupalia kweli kweli Urusi anata kuvamia Ukraine wakati mrusi hata kusema anavamia hajasema sasa propaganda zao zimegonga mwamba
Alikusudia kweli kuivamia Ukraine yakamshinda. Habari ndio hiyo!
 
Acheni propaganda nyie warusi wa Mbagala kwa mfuga nyoka 🐍 Russia katu haiwezi kuivamia Ukraine, akifanya hivyo nchi nzima wanaweza wakaokota makopo, wao wanalijua hilo vizuri sana.

Kwa ule uchumi wa Russia wakikaa vitani wiki mbili hakuna tena kitu uchumi wote utakuwa umesambaratika kabisa, vita sio mchezo.

Marekani bila kujihusisha na vita vya Iraq na Afghanistan leo hii uchumi wao ungekuwa mara mbili ya ulivyo sasa, ule wa China ungekuwa unaingia kwao mara mbili kabisa. Vita sio mchezo na Russia wanalifahamu hilo tena vizuri zaidi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] RUSSIA BHANA[emoji1787][emoji1787]
 
"Urusi aliwahi kuivamia Afghanistan akaikalia kwa miaka kumi. Nchi zilizokwenda kusaidia Afghanistan ili kumtoa Urusi ni Marekani na NATO,China, Pakistan,Saudi Arabia akiwasapoti kiuchumi akia Bin Laden na vitaifa vingine vidogovidogo.Lakini Mwamba alikaa miaka Kumi Hadi alipoamua kuondoa majeshi yake yaliyokuwepo Afghanistan na sehemu nyingine duniani baada ya kuona gharama ni kubwa mno za kuyahudimia majeshi"


Unajua msoto waliopata pale Afganistan. Wale mujahedeen ni balaa sana
 
"Urusi aliwahi kuivamia Afghanistan akaikalia kwa miaka kumi. Nchi zilizokwenda kusaidia Afghanistan ili kumtoa Urusi ni Marekani na NATO,China, Pakistan,Saudi Arabia akiwasapoti kiuchumi akia Bin Laden na vitaifa vingine vidogovidogo.Lakini Mwamba alikaa miaka Kumi Hadi alipoamua kuondoa majeshi yake yaliyokuwepo Afghanistan na sehemu nyingine duniani baada ya kuona gharama ni kubwa mno za kuyahudimia majeshi"


Unajua msoto waliopata pale Afganistan. Wale mujahedeen ni balaa sana
Acha Kudanganya watu wewe. Urusi aliondoa Majeshi yake nchini Afghanistan baada ya Marekani kuwapelekea Mujahideen Siraha. Moja ya Siraha hizo ni STINGER Anti-Aircraft Missiles. Hizi zilitungua HELLICOPTER GUNSHIP Nyingi za Urusi mpaka Urusi akaacha kurusha Ndege kwenye Anga la Afghanistan.

Baada ya hapo,Urusi alikuja na Vifaru. Hapo Mujahideen wakazidiwa Sana na Urusi ikateka maeneo mengi ya Mashariki mwa Afghanistan ambayo yanapakana na Urusi. Ndipo CIA wakatoa mafunzo ya Kijeshi kwa Mujahideen hao ya jinsi ya kutumia Siraha Aina ya JAVERINE.

Baada ya Hapo,Marekani alimwaga makontena ya JAVERINE anti-Tank Missiles. Wewe acha kabisa,Vifaru zaidi ya 300 vya Urusi viligeuzwa kuwa wajivu kabisa.

Baada ya Hapo Urusi haikuwa na Chaguo Bali kuondoka TU Afghanistan.
 
Vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vimeshupalia kweli kweli Urusi anata kuvamia Ukraine wakati mrusi hata kusema anavamia hajasema sasa propaganda zao zimegonga mwamba
Zime zaa matunda Urussi ilikuwa inajua Ukraine Hana backup nchi zote zenye nguvu zipo nyuma ya Ukraine saiv.
 
Back
Top Bottom