Inadaiwa huyu ndiye Moses Lijenge (luhende)

Inadaiwa huyu ndiye Moses Lijenge (luhende)

tozi zee

Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
20
Reaction score
73
Nimeona picha ikizunguka mtandaoni watu wanaomba wamuone mahakamani naye apandishwe kizimbani.

Narudia tena: INADAIWA kuwa ndiye yeye.

lunjenje.jpg


Utata umeibuka alipo mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kufadhili ugaidi inayomhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, aitwaye Moses Lijenge kama yuko hai au amefariki dunia.

Utata huo umeibuliwa leo Jumanne Septemba 28, 2021 na shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Mohamed Ling'wenya wakati akihojiwa na mawakili .

Shahidi huyo ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo anatoa ushahidi kwa lengo la kujiridhisha uhalali wa utoaji wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa ambayo mawakili wa utetezi walipinga yasipokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka wakidai yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria na mshtakiwa huyo alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na kutishiwa.

Awali, shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai aliieleza mahakama kuwa wakati wakiwakamata watuhumiwa wawili huko Moshi, mtuhumiwa wa tatu Lijenge hawakumpat, licha ya kumtafuta sehemu mbalimbali, hivyo wakaamua kuwapeleka Dar es Salaam watuhumiwa hao wawili.

Lakini katika ushahidi wake wa msingi jana, shahidi huyo alidai wakati wakitolewa kituo cha polisi kwenda Mbweni mmoja wa maaskari alimweleza kuwa mwenzake Moses Lijenge wameshamtupa kwa sababu alijidai kuwakimbia.

Alipohojiwa na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala leo Jumanne shahidi huyo amedai alivyoelezwa na askari yule kuwa mwenzao Lijenge wameshamtupa alielewa kuwa ameshauawa.

Akihojiwa zaidi na Kibatala, Mohamed amedai hajawahi kumsikia akitajwa mahali popote na upande wa mashtaka kama Lijenge ataunganishwa katika kesi hiyo, hivyo hajui kwa hakika kama yuko hai au ameshafariki.

Kwa sasa shahidi huyo wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo anaendelea kuhojiwa na upande wa mashtaka kuhusiana na ushahidi wake.

Chanzo: Mwananchi 28. 09. 2021
 
Shahidi alisema alitumia neno wameshamtupa. Kwa maoni yangu ni kwamba walimtesa hadi akafa na wakaamua kwenda kumtupa ili mwili wake usionekane.

Kuna haja ya kuwatafuta ndugu zake wa karibu ili kujua huyu jamaa kama bado yuko hai, wanajua alipo na kama hawajui Serikali itwambie Watanzania yuko wapi.

kupotezwa inamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom