Inadaiwa Kanisa ndo limepelekea mauaji ya Waziri Mkuu mstaafu Shinzo Abe

Inadaiwa Kanisa ndo limepelekea mauaji ya Waziri Mkuu mstaafu Shinzo Abe

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Huko Japan, kuna jamaa anaitwa Sun Myung Moon huyu mtu ndiye mwanzilishi wa Kanisa liitwalo Unification Church, al-maarufu kama Moonies church.

Huyu jamaa na kanisa lake ndiye chanzo cha mauaji ya Waziri Mkuu mstaafu wa Japan, Shinzo Abe.

Kwa mujibu wa Tetsuya Yamagani, ambaye ndiye aliyemuaa Shinzo Abe ni kwamna anamtuhumu Waziri Mkuu huyu kwa kuliunga mkono kanisa hilo katika kufanya shughuli zake nchini humo amnapo ilipelekea mwanzilishi kumfikia mama yake ili kulisaidia kanisa hilo.

Mama wa Tetsuya alianza kutumia pesa za familia kupeleka kama michango kulisaidia kanisa hilo huku wao wakikutana na changamoto kadhaa za kufedha kwa hatua hiyo ya mama yao.

Ndipo Tetsuya aliamua kumuwinda Shinzo Abe na kutimiza azma yake hiyo.

Kuna cha kujifunza hapa, kama hutaki acha

Credit Musembi
Britanicca
 
Upo sawa, jamaa aliachishwa kazi na akawa anategemea pesa za kiinua mgongo Cha mama yake, na Mwamp...... WA huko akafanya yake kuwarubuni waumini wapeleke majitolea!! hivyo kijana kabaki Kapa (Hana mia)!! Badala ya kumtafuta mwenye kanisa akaamua kumtafuta muumini aliyekuwa na Mamlaka ya kulifungia au kulifuta kanisa hilo
 
Huyo jamaa ni mbinafsi na muuaji tu,Kama Abe alisaidia kanisa kufanya kazi kosa lake nini?maana kupitia kanisa watu watapona roho zao,halafu mtu mwenye miaka 41 hela za Mamayake zinamhusu nini?

Huyo angeweza kumuua hata mama yake ili arithi pesa.
 
Britanicca unakuwa mwepesi kiasi hiki? Dah! Sikutegemea.
 
Ingekuwa ni rahisi hivyo, basi watu mashuhuri wengi wangekuwa wameisha duniani. Ni watu wangapi huuudhiwa na viongozi?
 
Mbona wanasema alikuwa mwanajeshi mstaafu,na baada ya mauaji alipokamatwa huyo muuaji aliulizwa kwa nini alifanya hivyo akajibu alikuwa hampendi marehemu.
 
Back
Top Bottom