NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Ni picha iliyojizolea umaarufu mkubwa watu wengi wakidhani picha hio ilikuwa ni ya kweli na ilipigwa kwa lengo la kumbukumbu, Stori ipo tofauti kabisa.
Picha hii imeandaliwa kwajili ya mikakati ya kutangaza na kuifanyia promoshen kampuni kubwa ya nguo "luis vutton", kampuni hii iliingia mkataba na wachezaji hawa na kuwalipa pesa ndefu ili wawe kwenye picha moja.
Wawili hao walikubali mkataba huo ila kwenye kupiga picha hawakuweza kupiga pamoja kirahisi, ilibidi Messi aende kwa muda wake na baada ya kuondoka akaja Ronaldo nae akapiga kivyake, baada ya hapo wataalam wa photoshop ndio wakaziunganisha.
Kwa makubaliano ya mkataba iliwabidi wote waposti kwa pamoja picha hio kwenye mitandao yao ya kijamii.
Hivyo si kama watu wengi wanavyodhani kwamba picha iliyopigwa ilikuwa wapo pamoja ama walipiga kishkaji iwe kumbukumbu kwao.
Kutokuwa na mazoea ndio chanzo kikuu
Ikumbukwe Ronaldo hakumpigia kura Messi kwenye Balon D' Or ya mwaka juzi.
Wawili hao hakuna aliye mfollow mwenzake kwenye mitandao ya kijamii