Tetesi: Inadaiwa yupo safe house

Time to pay for the evils he committed....
 
Kama ni dishi kuyumbiswa ni sawa, ila swala la kusema kwamba utameza vidonge ili usahau vitu selectively ni uongo.

Kwamfani Diwani amezeshwe vidonge vya kumfanya asahau yale yaliyohusu kazi yake bila kuathiri mengine yote, ni story tu
Mbona hushangai mtu anaumwa tumbo na kichwa lakini akipewa vidonge vya kutuliza kichwa pekee ndicho kitakachotulia na tumbo litaendelea kuuma.
 
I know you've got a handle!

SAWA.
Kati ya hizo 'receptors' zenyewe, tunaendelea kuzichambua utofauti kati yao, na 'selectively' tunazizaba zile zenye kumbukumbu ya maswala hayo ya kikazi.

utaendelea hivyo hivyo hadi tunapata zenyewe hasa, bila ya kuathiri zinazohusika na maswala mengineyo.
 
Hadi Samia sasa haoni shida kusema yeye anavyombo hivyo na anavitumia anavyotaka.
Rejea aliyosema alipokutana hivi karibuni na vyama vingine vya siasa.

Tabia hii ndiyo inayotakiwa kukataliwa kabisa katika Katiba Mpya.

Hivi vyombo ni vya waTanzania, siyo vya mtu binafsi au chama maalum.
 
Huna unalolijua. Unajua kuna watu humu baba zao,mama zao,kaka zao,dada zao ama ndugu zao wapo huko na tunaishi nao na kila kitu tunakijua kuwahusu? Au unadhani ni malaika wanatoka mbinguni!Niishie hapa.
 
Huna unalolijua. Unajua kuna watu humu baba zao,mama zao,kaka zao,dada zao ama ndugu zao wapo huko na tunaishi nao na kila kitu tunakijua kuwahusu? Au unadhani ni malaika wanatoka mbinguni!Niishie hapa.
Kwa akili yako timamu unafkiri wenye ndugu na jamaa huko au wazazi huwa wanatoa hizo siri au kujua wanachofanya hao ndugu zao?!?! Huo ni uongo uliotukuka danganya Mafala! hao TISS wenyewe hata wake na mume zao hawajui kazi za wenza wao ije kuwa wewe third-party yaan hata sio part of the family😂😂😂

Hao wanatafutaga kujikweza kwa kudanganya vitu vingine havinaga hata tija kutafuta sifa pasi na kuijua hatari yake. TISS hasemi wala huwezi kumjua... kuna levels ukifika utajulikana tu kama lile jopo linalokaaga nyuma ya Rais, mabalozi na wakurugenzi au maafsa wakubwa wa idara!.. ila hawa wengine HAPANA!

Amka we kilaza...😂👍🏾
 
Kwahiyo hata wale wale wakurugenzi wa idara ndani ya tiss wanaofahamika na kila mtu ama na wenza wao ni siri hakuna mwanafamilia anayewajua wanafanya kazi gani?

Wale wanaotembea kwenye msafara wa Rais ambao wanafahamika unataka kusema kwamba familia zao haziwafahamu kazi wanazozifanya?

Tatizo lako umewafanya hao watu kama malaika wakati tunaishi nao mtaani na ni washkaji zetu.

Ama mpaka utajiwe fulani ni mshkaji wangu na yupo idarani ndo uamini?
 
Mbona hushangai mtu anaumwa tumbo na kichwa lakini akipewa vidonge vya kutuliza kichwa pekee ndicho kitakachotulia na tumbo litaendelea kuuma.

Mnatumia mifano mabayo haiendani na mukitadha wa kinachozungumziwa hapa.

Wewe unazungumzia tumbo na kichwa (sehemu mbili) wakati mimi ninazungumzia swala la kumbukumbu ambazo zinahifadhiwa kwenye sehemu moja ya ubongo (sio viungo viwili tofauti).

Umeze vidonge kisha viende kwenye sehemu inayotunza kumbukumbu, halafu ikachague kufuta zile zinazohusu kazi fulani bila kuathiri kumbukumbu nyingine? How comes vidonge vinakuwa selective kwenye kufuta kumbukumbu??

Unless kuwe na njia nyingine inayoweza kuchagua vya kufuta lakini sio kumeza vidonge, HAIWEZEKANI.
 


Mkuu unless kuna namna nyingine ya kuzichambua (kwakua technology imekuwa), lakini si kumeza vidonge?

Hata ukitulia kwa makini utagundua kuwa hicho ulicho-suggest hapa, hatuwezi kukifanikisha kwa kumeza vidonge.
 
Mkuu unless kuna namna nyingine ya kuzichambua (kwakua technology imekuwa), lakini si kumeza vidonge?

Hata ukitulia kwa makini utagundua kuwa hicho ulicho-suggest hapa, hatuwezi kukifanikisha kwa kumeza vidonge.
Kwani tatizo ni lipi mkuu 'Mac Alpho', "vidonge" ni 'metaphor', tu. Kama hutaki hilo neno "vidonge", basi tumia neno "targeted drug delivery", kwenye eneo husika panapotakiwa hiyo dawa ipafanyie kazi.

Kwa hiyo, katika mfano huu, mtu anaweza akameza vidonge ambavyo vimebeba dawa mahususi inayokwenda kuzizaba 'receptors' maalum ndani ya ubongo zinazojishughulisha na maswala ya kumbukumbu za mambo fulani yanayomhusu mhusika.

Au kama hupendelei njia hiyo ya vidonge, basi, tutaiwasilisha hiyo dawa karibu kabisa na mahali pake pa kufanyia kazi, ndani ya ubongo wenyewe, kwa njia mbalimbali, badala ya vidonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…