Tetesi: Inadaiwa yupo safe house

Tetesi: Inadaiwa yupo safe house

Inadaiwa baada ya kupekuliwa amekamatwa na kuwekwa safe house kama walivyofanya kwa Kapilimba.

Mtu anapekuliwa na kukaguliwa na lengo kuvunjwa zile connection zote akitoka hapo ata line za simu atasajili zingine na kuanza Maisha mapya.

Tunakuombea buddy hata kama uliwaumiza ndugu zetu🙏🙏
Time to pay for the evils he committed....
 
Kama ni dishi kuyumbiswa ni sawa, ila swala la kusema kwamba utameza vidonge ili usahau vitu selectively ni uongo.

Kwamfani Diwani amezeshwe vidonge vya kumfanya asahau yale yaliyohusu kazi yake bila kuathiri mengine yote, ni story tu
Mbona hushangai mtu anaumwa tumbo na kichwa lakini akipewa vidonge vya kutuliza kichwa pekee ndicho kitakachotulia na tumbo litaendelea kuuma.
 
Haya yote niliyaelewa ndiomaana nikaja na hoja ya kupinga mkuu.

Huko kwenye ubongo kuna receptors zinazohusika na kumbukumbu in general, kwahiyo kama ni kuzigusa moja kwa moja ni lazima uharibu kumbukumbu zake in general.

Hakuna namna unaweza kuniambia dawa (vidonge), vitaenda kuharibu kumbukumbu zake zinazohusu kazi yake (aliyostafishwa) bila kuathiri kumbukumbu zake nyingine.

NB: Hatuwezi kufuta memory yake kuhusu kazi zake selectively bila kuathiri nyinginezo, labda kama tunazungumzia kuutia dhoruba kidogo sana mfumo wake wa kumbukumbu(wote kwa ujumla) ili akose mpangilio maalumu kila akijaribu kufikiri. Na madhara yake ni lazima yaonekane tu.
I know you've got a handle!

SAWA.
Kati ya hizo 'receptors' zenyewe, tunaendelea kuzichambua utofauti kati yao, na 'selectively' tunazizaba zile zenye kumbukumbu ya maswala hayo ya kikazi.

utaendelea hivyo hivyo hadi tunapata zenyewe hasa, bila ya kuathiri zinazohusika na maswala mengineyo.
 
Hii ndiyo changamoto mojawapo ya usalama wa nchi kugeuka kuwa usalama wa 'regime'. Tumeshuhudia kwa macho yetu jinsi kila kiongozi anayeshika madaraka anavyofanyia vyombo vya ulinzi na usalama mageuzi kwa mapenzi yake tu! Raia wamepotezwa ikiwa ni pamoja na kuondolewa uhai ili tu kulinda udhaifu wa wanasiasa walioshika madaraka. Vyombo hivi vinahitaji kuwa vya kikatiba zaidi kuliko kuwa vya kisiasa. Katiba bora ndiyo usalama wa kila raia, kila taasisi ya umma na kila kitu.
Hadi Samia sasa haoni shida kusema yeye anavyombo hivyo na anavitumia anavyotaka.
Rejea aliyosema alipokutana hivi karibuni na vyama vingine vya siasa.

Tabia hii ndiyo inayotakiwa kukataliwa kabisa katika Katiba Mpya.

Hivi vyombo ni vya waTanzania, siyo vya mtu binafsi au chama maalum.
 
Hehe! Sio TISS hao wanakudanganya... TISS hawana njaa za hovyo wala si rahisi kulaghaiwa na kina mwenzangu na mimi. Yeah! Ni watu kama wewe lakini sio kama wewe hayo mawazo ya hovyo ondoa! Na ni wambea sawa ila ni wambea wenye kushughulika na umbea wenye tija na manufaa kwa kunusuru maslahi ya taifa kwa ujumla. Mpaka umekaa hapo kwenye kochi la mtumba na unaharisha tu maneno ya kashfa kumbuka kuna wanaume hawana huo muda hata wa kuzungumza na ndugu na vipenzi vyao ili wewe ule mema ya nchi na utafute rizq yako kwa amani... unakuja kuwakashifu.. dahh! Bin-Adam bana [emoji4][emoji4]☻
Huna unalolijua. Unajua kuna watu humu baba zao,mama zao,kaka zao,dada zao ama ndugu zao wapo huko na tunaishi nao na kila kitu tunakijua kuwahusu? Au unadhani ni malaika wanatoka mbinguni!Niishie hapa.
 
Huna unalolijua. Unajua kuna watu humu baba zao,mama zao,kaka zao,dada zao ama ndugu zao wapo huko na tunaishi nao na kila kitu tunakijua kuwahusu? Au unadhani ni malaika wanatoka mbinguni!Niishie hapa.
Kwa akili yako timamu unafkiri wenye ndugu na jamaa huko au wazazi huwa wanatoa hizo siri au kujua wanachofanya hao ndugu zao?!?! Huo ni uongo uliotukuka danganya Mafala! hao TISS wenyewe hata wake na mume zao hawajui kazi za wenza wao ije kuwa wewe third-party yaan hata sio part of the family😂😂😂

Hao wanatafutaga kujikweza kwa kudanganya vitu vingine havinaga hata tija kutafuta sifa pasi na kuijua hatari yake. TISS hasemi wala huwezi kumjua... kuna levels ukifika utajulikana tu kama lile jopo linalokaaga nyuma ya Rais, mabalozi na wakurugenzi au maafsa wakubwa wa idara!.. ila hawa wengine HAPANA!

Amka we kilaza...😂👍🏾
 
Kwa akili yako timamu unafkiri wenye ndugu na jamaa huko au wazazi huwa wanatoa hizo siri au kujua wanachofanya hao ndugu zao?!?! Huo ni uongo uliotukuka danganya Mafala! hao TISS wenyewe hata wake na mume zao hawajui kazi za wenza wao ije kuwa wewe third-party yaan hata sio part of the family[emoji23][emoji23][emoji23]

Hao wanatafutaga kujikweza kwa kudanganya vitu vingine havinaga hata tija kutafuta sifa pasi na kuijua hatari yake. TISS hasemi wala huwezi kumjua... kuna levels ukifika utajulikana tu kama lile jopo linalokaaga nyuma ya Rais ila hawa wengine HAPANA!

Amka we kilaza...[emoji23][emoji1474]
Kwahiyo hata wale wale wakurugenzi wa idara ndani ya tiss wanaofahamika na kila mtu ama na wenza wao ni siri hakuna mwanafamilia anayewajua wanafanya kazi gani?

Wale wanaotembea kwenye msafara wa Rais ambao wanafahamika unataka kusema kwamba familia zao haziwafahamu kazi wanazozifanya?

Tatizo lako umewafanya hao watu kama malaika wakati tunaishi nao mtaani na ni washkaji zetu.

Ama mpaka utajiwe fulani ni mshkaji wangu na yupo idarani ndo uamini?
 
Mbona hushangai mtu anaumwa tumbo na kichwa lakini akipewa vidonge vya kutuliza kichwa pekee ndicho kitakachotulia na tumbo litaendelea kuuma.

Mnatumia mifano mabayo haiendani na mukitadha wa kinachozungumziwa hapa.

Wewe unazungumzia tumbo na kichwa (sehemu mbili) wakati mimi ninazungumzia swala la kumbukumbu ambazo zinahifadhiwa kwenye sehemu moja ya ubongo (sio viungo viwili tofauti).

Umeze vidonge kisha viende kwenye sehemu inayotunza kumbukumbu, halafu ikachague kufuta zile zinazohusu kazi fulani bila kuathiri kumbukumbu nyingine? How comes vidonge vinakuwa selective kwenye kufuta kumbukumbu??

Unless kuwe na njia nyingine inayoweza kuchagua vya kufuta lakini sio kumeza vidonge, HAIWEZEKANI.
 
I know you've got a handle!

SAWA.
Kati ya hizo 'receptors' zenyewe, tunaendelea kuzichambua utofauti kati yao, na 'selectively' tunazizaba zile zenye kumbukumbu ya maswala hayo ya kikazi.

utaendelea hivyo hivyo hadi tunapata zenyewe hasa, bila ya kuathiri zinazohusika na maswala mengineyo.


Mkuu unless kuna namna nyingine ya kuzichambua (kwakua technology imekuwa), lakini si kumeza vidonge?

Hata ukitulia kwa makini utagundua kuwa hicho ulicho-suggest hapa, hatuwezi kukifanikisha kwa kumeza vidonge.
 
Mkuu unless kuna namna nyingine ya kuzichambua (kwakua technology imekuwa), lakini si kumeza vidonge?

Hata ukitulia kwa makini utagundua kuwa hicho ulicho-suggest hapa, hatuwezi kukifanikisha kwa kumeza vidonge.
Kwani tatizo ni lipi mkuu 'Mac Alpho', "vidonge" ni 'metaphor', tu. Kama hutaki hilo neno "vidonge", basi tumia neno "targeted drug delivery", kwenye eneo husika panapotakiwa hiyo dawa ipafanyie kazi.

Kwa hiyo, katika mfano huu, mtu anaweza akameza vidonge ambavyo vimebeba dawa mahususi inayokwenda kuzizaba 'receptors' maalum ndani ya ubongo zinazojishughulisha na maswala ya kumbukumbu za mambo fulani yanayomhusu mhusika.

Au kama hupendelei njia hiyo ya vidonge, basi, tutaiwasilisha hiyo dawa karibu kabisa na mahali pake pa kufanyia kazi, ndani ya ubongo wenyewe, kwa njia mbalimbali, badala ya vidonge.
 
Back
Top Bottom