KWELI Inaelezwa kucheka ni tiba na huimarisha afya ya mwili

KWELI Inaelezwa kucheka ni tiba na huimarisha afya ya mwili

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Nimekutana na huu ujumbe Facebook je, kinachozungumzwa ni cha kweli?

Kucheka si tu ishara ya furaha — ni tiba ya mwili na akili pia! Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa kucheka husaidia kupunguza msongo wa mawazo (stress), huimarisha kinga ya mwili, na hata kuboresha afya ya moyo.

Wanasayansi wanasema kwamba dakika chache tu za kucheka kwa dhati huongeza utoaji wa endorphins — kemikali za furaha mwilini — na pia hupunguza maumivu ya mwili.


1783846828366.png
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa Bugando Magazine kutoka hospitali ya Bugando linaeleza kuwa hospitali nyingine duniani zina "vyumba vya kucheka" kwa wagonjwa kwani kucheka kwa dakika 10 kwa siku kunapunguza homoni za msongo na kuongeza kinga ya mwi-li.

Kulingana na daktari bingwa wa saratani Edward T. Creagan wa Mayo Clinic, kucheka hupunguza homoni za msongo kama cortisol na epinephrine huku kukiongeza homoni zinazohusishwa na hisia za furaha na ustawi, ikiwemo endorphins, dopamine na oxytocin. Hali hii husaidia kupunguza msongo wa mawazo, dalili za wasiwasi na unyogovu, kuboresha kumbukumbu, ubunifu, mawasiliano na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.

Mbali na afya ya akili, kucheka kunaweza pia kuchangia afya ya mwili kwa kusaidia kupunguza shinikizo la damu, kuboresha mzunguko wa damu, kulegeza misuli, kupunguza maumivu na kuimarisha utendaji wa mfumo wa kinga.

Aidha anaeleza kuwa tafiti pia zinaonyesha kuwa watu wanaocheka mara kwa mara wanaweza kuwa na afya bora wanapozeeka na kupunguza hatari ya kupata ulemavu wa utendaji. Wataalamu wanashauri kujumuisha vichekesho na mazungumzo ya kufurahisha katika maisha ya kila siku, huku wakisisitiza kuwa ucheshi unapaswa kuwa wa kujenga na usiowadharau au kuwaumiza wengine.

Vilevile tovuti ya National Library of Medicine inaeleza kuwa kucheka kuna manufaa mbalimbali kwa afya ya mwili na akili. Kicheko kizuri husaidia kulegeza misuli na kupunguza msongo wa mawazo kwa muda, huku kikichochea utolewaji wa endorphins homoni zinazoongeza hisia za furaha na kupunguza maumivu kwa muda. Pia, kucheka hupunguza homoni za msongo na kunaweza kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuongeza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi.

Aidha, tafiti zinaonyesha kuwa kucheka kunaweza kuboresha mtiririko wa damu na afya ya moyo, kuchoma kiasi kidogo cha kalori, na kusaidia kudumisha afya ya akili kwa kuongeza mtazamo chanya hata wakati wa changamoto. Kwa ujumla, kucheka mara kwa mara ni njia rahisi inayoweza kuchangia ustawi wa mwili na akili, ingawa si mbadala wa matibabu au mtindo bora wa maisha.​
Back
Top Bottom