Inafaa ichezewe filamu?

Inafaa ichezewe filamu?

Groxygone

Member
Joined
Oct 10, 2026
Posts
11
Reaction score
6

UYUNU​


Rafiki Ambaye Haniachi​


Aina: story ya kisaikolojia
Mhusika mkuu: Uyunu, msichana wa miaka 17
Rafiki yake: Neema




1​

NDANI — DARASANI — SAA KUMI KASORO (15:50)


Mwalimu amesimama mbele ya darasa akifundisha. Wanafunzi wanamsikiliza, lakini Uyunu amekaa kimya, akiwa amezama katika mawazo.


Mwalimu anaandika swali ubaoni, kisha anageuka.


MWALIMU:
Uyunu, simama. Nijibu swali hili.


Uyunu anainua kichwa.


UYUNU:
Ndiyo, mwalimu.


MWALIMU:
Basi, jibu ni lipi?


Uyunu anatazama ubaoni. Anajaribu kutafuta jibu, lakini anashindwa kuzungumza.


MWALIMU:
Uyunu, umesikia nilichokuuliza?


UYUNU:
Ndiyo, mwalimu.


MWALIMU:
Kwa hiyo, kwa nini hujibu?


Uyunu anabaki kimya.


Wanafunzi wachache wanaanza kucheka.


Neema, aliyekaa upande mwingine wa darasa, anacheka pamoja nao.


Uyunu anamtazama Neema kwa muda mfupi. Anaonek

Binti mmoja, ambaye ni mtoto wa mwalimu, hamcheki Uyunu. Anamtazama kwa huruma.


MWALIMU:
Sawa, kaa chini. Lakini unatakiwa kuwa makini na masomo yako.


Uyunu anakaa bila kusema chochote.


Mwalimu anaendelea kufundisha, lakini Uyunu haonekani tena kufuatilia somo.


Hatimaye, kengele ya mwisho inalia.




2​

NDANI — DARASANI — SAA KUMI ALASIRI (16:00)


Wanafunzi wanaanza kufunga madaftari na kukusanya mabegi yao.


Darasa linajaa mazungumzo na vicheko.


MWANAFUNZI 1:
Kesho msije mkachelewa tena!


MWANAFUNZI 2:
Wewe ndiye huwa unachelewa kila siku!


Wanafunzi wanacheka na kutoka.


Uyunu naye anafunga daftari lake, kisha anachukua begi lake.


Anapolirusha begi begani, anasikia sauti nyuma yake.


NEEMA:
Boo!


Neema anamgusa begani ghafla.


Uyunu anashtuka na kugeuka kwa haraka.


Neema anacheka kwa furaha.


NEEMA:
Dah! Umeona ulivyoruka? Nilidhani ungeenda mpaka ofisini kwa mwalimu!


Uyunu hamcheki.


Neema anapunguza kicheko chake.


NEEMA:
Mbona hivyo tena? Nilikuwa nakusalimia tu!


Anasogea na kujaribu kumchukulia Uyunu begi.


NEEMA:
Hebu nipe begi lako nikusaidie kubeba. Leo nimeamua kuwa mtu mwema.


Uyunu analivuta begi lake na kulikumbatia.


UYUNU:
Usiniguse.


Neema anamtazama kwa mshangao.


NEEMA:
Kwani nimefanya nini?


UYUNU:
Nimesema usiniguse. Nenda zako, Neema.


NEEMA:
Uyunu, kuna nini?


UYUNU:
Unaniuliza kuna nini? Ulipokuwa unacheka na wenzako niliposhindwa kujibu swali, hukujua kuna nini?


Neema ananyamaza.


NEEMA:
Nilikuwa...


UYUNU:
Sitaki kusikia. Kama unaona ni raha kunicheka mbele ya watu, basi nenda ukae na hao unaocheka nao.


NEEMA:
Lakini Uyunu, mimi ni rafiki yako.


UYUNU:
Basi acha kunifuata! Tafuta rafiki mwingine.


Uyunu anageuka na kuelekea mlangoni.


NEEMA:
Uyunu, subiri kidogo!


UYUNU:
Niache!


Uyunu anatoka darasani bila kuangalia nyuma.


Neema anabaki amesimama kwa muda. Kisha anachukua begi lake na kutoka pia.




3​


NDANI — DARASANI — BAADA YA SAA KUMI


Uyunu anarudi darasani na kukaa kwenye kiti chake.


Darasa sasa ni tupu.


Analiweka begi lake pembeni na kutazama dawati lililo mbele yake.


Anakumbuka namna wanafunzi walivyomcheka, kisha anakumbuka jinsi Neema alivyojiunga nao.


Anainamisha kichwa.


Muda unapita.


Sauti za wanafunzi wanaoondoka shuleni zinazidi kupungua. Hatimaye, uwanja unakuwa kimya.


Mwanga wa mchana unaanza kupungua.


Uyunu bado amekaa darasani.


BAADAYE — NJE YA DARASA​


Mlinzi anapita akikagua madarasa.


Anapoona Uyunu bado yupo, anasimama mlangoni.


MLINZI:
Wewe binti! Bado upo hapa?


Uyunu anainua kichwa.


UYUNU:
Ndiyo, mzee.


MLINZI:
Unasubiri nani? Shule imefungwa tangu muda mrefu.


UYUNU:
Simsubiri mtu.


MLINZI:
Basi unafanya nini hapa mpaka muda huu? Toka nje, tunataka kufunga geti.


Uyunu anachukua begi lake na kusimama.


UYUNU:
Sawa, mzee.


MLINZI:
Na kesho usije ukabaki mpaka giza. Ukiwa na tatizo, tafuta mwalimu akusaidie kabla hawajaondoka.


Uyunu anatikisa kichwa na kuanza kutembea kuelekea getini.




5​


NJE — GETI LA SHULE — GIZA LINAKARIBIA


Uyunu anatoka nje ya geti na kuanza kutembea kuelekea nyumbani.


Barabara imetulia. Anarekebisha begi lake begani huku akitembea peke yake.


Ghafla, anasikia sauti nyuma yake.


NEEMA (AKIWA MBALI):
Uyunu! Nisubiri!


Uyunu anaendelea kutembea.


NEEMA:
Uyunu! Nasema nisubiri!


Neema anakuja kwa haraka, begi lake likiruka-ruka mgongoni.


NEEMA:
Jamani! Miguu yako ina injini gani? Simama basi!


Uyunu anageuka kidogo.


Neema anamfikia akiwa anavuta pumzi.


NEEMA:
Dah! Unataka kuniua kwa kunitembeza hivi? Hata ungeweza kusubiri niseme jambo moja tu!


UYUNU:
Kwa nini umekuja tena?


NEEMA:
Kwa sababu nilikuambia nisubiri, lakini wewe unatembea kana kwamba unakimbizwa na polisi!


Uyunu anageuka na kuendelea kutembea.


Neema anamfuata.


NEEMA:
Sawa, nimekuelewa. Leo umenikasirikia.


UYUNU:
Kama umenielewa, kwa nini umekuja?


NEEMA:
Kwa sababu hasira yako haijafuta urafiki wetu.


Uyunu anabaki kimya.


Neema anapunguza sauti yake.


NEEMA:
Uyunu, nisikilize. Samahani kwa nilichofanya darasani. Sikufikiria kwamba kucheka kwangu kungekuumiza hivyo.


Uyunu haongei.


NEEMA:
Nilipaswa kukutetea, au angalau nibaki kimya. Lakini nilijiunga na wengine. Nilikosea.


UYUNU:
Ulinifanya nijisikie vibaya sana.


NEEMA:
Najua. Naomba unisamehe.


Kimya kinatawala kwa muda.


Neema anamtazama rafiki yake kwa upande wa jicho.


NEEMA:
Kama hutaki kunisamehe leo, sawa. Lakini tafadhali usinihukumu kifungo cha maisha. Mimi bado nina ndoto za kuolewa!


Uyunu anageuka kumtazama.


UYUNU:
Wewe? Nani atakuoa?


Neema anasimama ghafla na kushika kifua.


NEEMA:
Aisee! Kwa hiyo unaona mimi sistahili kuolewa?


UYUNU:
Sijasema hivyo.


NEEMA:
Umesema kwa macho yako! Hata macho yako yananidharau!


Uyunu anashindwa kujizuia na kucheka kidogo.


Neema anaonyesha kidole chake.


NEEMA:
Aha! Nimeona! Umecheka! Basi bado nina nafasi moyoni mwako!


UYUNU:
Usijisifie. Nimecheka kwa sababu ya ujinga wako.


NEEMA:
Hata kama ni ujinga wangu, mradi nimefanikiwa kukufanya ucheke.


Uyunu anatabasamu kidogo.


UYUNU:
Unaahidi hutafanya tena?


Neema anainua mkono wake.


NEEMA:
Naapa kwa daftari langu la hesabu!


UYUNU:
Daftari lako ambalo hata huandiki chochote?


Neema anasimama na kumtazama kwa mshangao.


NEEMA:
Wewe! Hata katika kipindi hiki cha kuomba msamaha unataka kunivunjia heshima?


UYUNU:
Nakwambia ukweli.


NEEMA:
Basi kiapo changu ni kizito zaidi. Hata daftari langu lenyewe likisikia, litajaza kurasa zake kwa hofu!


Uyunu anacheka.


Wanaanza kutembea pamoja.




5​

NJE — BARABARANI — JIONI


Neema anatembea kwa uchangamfu pembeni ya Uyunu. Mara nyingine anaenda hatua chache mbele, kisha anarudi ili waweze kutembea pamoja.


NEEMA:
Uyunu, kuna kitu nataka kukuuliza.


UYUNU:
Uliza.


NEEMA:
Kwani wewe huwa unafurahia kuwa mkimya hivyo, au unalipwa kwa kila neno unalookoa?


UYUNU:
Neema, nimeanza kujuta kukusamehe.


NEEMA:
Hapana, usijute! Ngoja nimalize.


Anamwangalia Uyunu kwa makini.


NEEMA:
Unajua watu wengi wanavyokuona?


UYUNU:
Wananionaje?


NEEMA:
Wanasema una kiburi. Wengine wanafikiri unajiona bora kuliko wao. Kuna hata wale wanaosema ukiwasalimia, unajibu kana kwamba wamekuomba pesa.


Uyunu anageuka kumtazama.


UYUNU:
Na wewe unafikiri hivyo?


Neema anatikisa kichwa.


NEEMA:
Mimi? Hapana kabisa.


UYUNU:
Kwa nini?


NEEMA:
Kwa sababu mimi nakujua. Watu wanakuona ukiwa kimya, wanafikiri unawadharau. Lakini mimi najua kuna wakati unakaa kimya kwa sababu una mambo mengi moyoni mwako.


Uyunu anapunguza mwendo.


UYUNU:
Na kama kweli nina kiburi?


NEEMA:
Basi ungekuwa na kiburi kwangu pia. Lakini angalia mimi ninavyokufuata kila siku kama kuku anayemfuata mwenye chakula!


Uyunu anacheka.


UYUNU:
Kwa hiyo wewe ni kuku?


NEEMA:
Kuku mwenye akili! Usinifananishe na wale wanaokimbia mvua bila kujua wanakimbilia wapi.


UYUNU:
Lakini wewe mwenyewe ukiona mvua unakimbia kuliko wote.


NEEMA:
Mimi nakimbia kwa sababu nina akili. Mvua ikinilowesha, sare yangu itakauka kwa gharama ya nani?


Uyunu anacheka zaidi.


Neema naye anacheka, kisha anakuwa mtulivu.


NEEMA:
Lakini nisikilize, Uyunu. Si lazima kila mtu akuelewe. Wengine watakuhukumu kwa jinsi wanavyokuona tu. Hawajui unachofikiria, wala hawajui mambo unayopitia.


UYUNU:
Wakati mwingine huwa natamani niwe mtu mwingine. Mtu ambaye watu wanampenda bila kumwelewa vibaya.


Neema anapunguza mwendo na kutembea sambamba naye.


NEEMA:
Usitamani kuwa mtu mwingine. Mimi nakupenda jinsi ulivyo.


Uyunu anamtazama.


UYUNU:
Hata nikiwa na huzuni?


NEEMA:
Ndiyo.


UYUNU:
Hata nisipotaka kuzungumza?


NEEMA:
Ndiyo.


UYUNU:
Hata nikikukasirikia kama nilivyokukasirikia leo?


Neema anajifanya kufikiria kwa makini.


NEEMA:
Hapo inategemea.


Uyunu anakunja uso.


UYUNU:
Inategemea nini?


NEEMA:
Kama umenikasirikia halafu unataka nikununulie chips, hapo urafiki wetu utakuwa umeingia kwenye mazungumzo magumu!


Uyunu anacheka na kumsukuma kwa upole.


UYUNU:
Wewe huna akili!


NEEMA:
Lakini bado unanipenda!


UYUNU:
Usijiamini sana.


NEEMA:
Sawa. Sitajiamini. Nitakuamini wewe badala yake.


Wanaendelea kutembea.


Baada ya muda, Uyunu ananyamaza tena.


UYUNU:
Neema?


NEEMA:
Naam, bibi yangu.


UYUNU:
Unafikiri siku moja watu watakuja kunielewa kweli?


Neema anamtazama kwa umakini.


NEEMA:
Huenda wasielewe kila kitu. Lakini huhitaji kila mtu akuelewe ili uwe na thamani. Cha muhimu ni kuwa na mtu mmoja ambaye hatakuhukumu kabla hajakusikiliza.


UYUNU:
Na wewe utakuwa mtu huyo?


Neema anatabasamu na kumshika mkono.


NEEMA:
Nitakuwa. Na siku ukisahau kwamba una mtu anayekujali, nitakufuata mpaka unisikie.


UYUNU:
Hata nikikufukuza?


NEEMA:
Nitakuja kesho.


UYUNU:
Na nikikufukuza tena?


NEEMA:
Nitakuja kesho kutwa!


Uyunu anacheka.


NEEMA:
Ila ukinifukuza kwa siku saba mfululizo, nitakuja na barua ya malalamiko kwa mama yako!


UYUNU:
Neema!


Wote wanacheka.


Baada ya muda, Uyunu anamtazama Neema kwa uzito.


UYUNU:
Neema, unaahidi hutaniacha?


Neema anasimama na kumtazama moja kwa moja.


Kwa mara hii, hatanii.


NEEMA:
Nakuahidi, Uyunu. Sitakuacha.


UYUNU:
Kweli?


NEEMA:
Kweli kabisa.


Neema anatabasamu, kisha anageuza mazungumzo.


NEEMA:
Sasa twende kabla hujaanza kuniuliza maswali ya mtihani!


Wanaendelea kutembea pamoja.
6

NJE — BARABARANI, KARIBU NA NYUMBA — JIONI


Uyunu na Neema wanaendelea na safari yao. Neema anatembea huku akizungumza, mara nyingine akicheza na mkanda wa begi lake.


Anapoona nyumba iliyo karibu, anapunguza mwendo.


NEEMA:
Uyunu, nisubiri kidogo. Naenda kukojoa.


UYUNU:
Sawa. Nipe begi lako nikushikilie.


Neema analikumbatia begi lake mara moja.


NEEMA:
Nikukabidhi begi langu? Wewe mwenyewe?


Uyunu anamtazama kwa mshangao.


UYUNU:
Sasa kuna tatizo gani?


NEEMA:
Hapana! Nakulipiza kisasi.


UYUNU:
Unanilipiza nini tena?


Neema anatabasamu kwa ushindi.


NEEMA:
Unakumbuka siku ile uliponifanya nibebe vitabu vyako pamoja na begi langu?


UYUNU:
Sasa ndiyo nini?


NEEMA:
Leo nimepata nafasi yangu. Nitabeba begi langu mwenyewe. Utaona jinsi ilivyo raha!


UYUNU:
Dah! Una kinyongo hata kuhusu begi?


NEEMA:
Ndiyo! Mimi si mtu wa kusahau mambo.


Uyunu anajaribu kulichukua begi kwa utani.


Neema analivuta haraka na kulificha nyuma yake.


NEEMA:
Usiniguse! Nenda ukatafute begi lako mwenyewe!


UYUNU:
Basi nenda zako, mjinga wewe.


Neema anacheka.


NEEMA:
Nitarudi muda mfupi. Usije ukatoroka na kuniacha hapa!


UYUNU:
Mimi ndiye nitoroke? Wewe ndiye unaenda zako!


Neema anaendelea kucheka huku akizunguka nyuma ya nyumba iliyo karibu.


NEEMA:
Nakuja sasa hivi!


Uyunu anabaki akimwangalia mpaka Neema anapotea nyuma ya nyumba.


Kisha anasubiri.


Sekunde zinapita.


Uyunu anarekebisha begi lake begani na kutazama upande ambao Neema ameondokea.


UYUNU:
Neema, unafanya nini muda wote huo?


Anacheka kidogo kana kwamba anazungumza na rafiki yake.


UYUNU:
Ukirudi nitakufanya ubebe begi langu mpaka nyumbani. Ndiyo kisasi changu!


Anasubiri tena.


Hakuna Neema.




SCENE YA 7: SIMU​


NDANI — NYUMBA — JIONI


Mama yake Uyunu yuko nyumbani pamoja na mjomba na baba mkubwa.


Simu inaita.


Mama anainua simu na kupokea.


MAMA:
Halo?


Anasikiliza.


Uso wake unabadilika.


MAMA:
Unasema nini? Yuko wapi sasa?


Anasikiliza tena, kisha anamtazama mjomba kwa hofu.


MAMA:
Anazungumza peke yake?


Mjomba anamsogelea.


MJOMBA:
Kuna nini?


Mama anashusha simu taratibu.


MAMA:
Wamesema Uyunu yuko njiani, anazungumza peke yake. Wamesema tumfuate haraka.


Baba mkubwa anasimama.


BABA MKUBWA:
Twende. Tusipoteze muda.


Wote wanaondoka kwa haraka.




SCENE YA 8: WANAMKUTA UYUNU​


NJE — BARABARANI — JIONI, KARIBU SAA KUMI NA MBILI (18:00)


Uyunu bado amesimama akimsubiri Neema.


Anatazama nyuma ya nyumba tena.


Anapogeuka, anawaona mama yake, mjomba na baba mkubwa wakimjia kwa haraka.


UYUNU:
Mama? Mnafanya nini huku?


Mama yake anamfikia na kumshika mkono.


MAMA:
Uyunu, mwanangu, ulikuwa unafanya nini hapa?


UYUNU:
Namsubiri Neema.


Mama anamtazama mjomba kwa hofu.


MJOMBA:
Neema yuko wapi?


Uyunu anaelekeza mkono nyuma ya nyumba.


UYUNU:
Ameenda kukojoa. Aliniambia nimsubiri, atarudi muda mfupi.


Wote wanageukia upande ambao Uyunu ameonyesha.


Kisha wanamtazama tena.


MAMA:
Mwanangu, twende nyumbani.


UYUNU:
Subiri Neema arudi kwanza.


MJOMBA:
Tutamtafuta baadaye. Twende sasa.


Uyunu anatikisa kichwa.


UYUNU:
Hapana. Siwezi kumuacha hapa. Tumetoka shuleni pamoja.


MJOMBA:
Uyunu, tafadhali, twende.


UYUNU:
Kwa nini mnanilazimisha? Neema yuko kule tu!


Baba mkubwa anawatazama mama na mjomba, akiona jinsi wanavyokuwa na wasiwasi.


Anainua mkono kuwazuia.


BABA MKUBWA:
Msimlazimishe! Ngoja tumsubiri rafiki yake.


MJOMBA:
Lakini...


BABA MKUBWA:
Nimesema tumsubiri. Tusimfanye aogope zaidi.


Wananyamaza.


Wanasimama pamoja na Uyunu, wakielekea kutazama nyuma ya nyumba.


Dakika moja inapita.


Dakika mbili.


Uyunu anaanza kuangalia saa yake.


Dakika tatu.


Anageuka kumtazama mama yake.


UYUNU:
Mbona hajarudi?


Mama yake hawezi kumjibu.


Dakika nne zinapita.


Uyunu anaanza kutembea kuelekea nyuma ya nyumba.


UYUNU:
Ngoja nikamwangalie. Huenda kuna kitu kimempata.


Mjomba anamsogelea.


MJOMBA:
Uyunu, usiende.


UYUNU:
Mbona? Ni rafiki yangu!


Anajaribu kupita.


Mama yake anamshika mkono.


UYUNU:
Mama, niache! Nataka kumwangalia Neema!


Baba mkubwa na mjomba wanamsogelea pia.


Uyunu anaanza kuwa na hofu.


UYUNU:
Mnafanya nini? Kwa nini mnanizuia?


Mama yake anajaribu kumkumbatia.


MAMA:
Mwanangu, tafadhali, twende nyumbani.


Uyunu anajitahidi kujitoa mikononi mwao.


UYUNU:
Hapana! Neema ananisubiri! Mnanizuia nini?


Mjomba anamshika kwa nguvu zaidi ili asikimbilie nyuma ya nyumba.


Uyunu anawaangalia mmoja baada ya mwingine. Macho yake yamejaa hofu na kuchanganyikiwa.


UYUNU:
Mnataka kunipeleka hospitalini?


Hakuna anayejibu.


UYUNU:
Mnafikiri nina wazimu?


Mama yake anaanza kulia kimyakimya.


UYUNU:
Sina wazimu! Neema yuko kule! Nyinyi wenyewe mmeniona nikimsubiri!


Baba mkubwa anajaribu kuzungumza naye kwa utulivu.


BABA MKUBWA:
Uyunu, mwanangu, tulia kwanza.


UYUNU:
Sitaki kutulia! Namtaka rafiki yangu!


Uyunu anajaribu tena kwenda nyuma ya nyumba, lakini mjomba anamzuia.


Mjomba anatoa simu yake na kupiga simu ya teksi.


Uyunu anapoona simu, anaaanaanza kulia

​

 
Back
Top Bottom