Maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya takriban watu 1,000 katika milima ya Marra magharibi mwa Sudan, kulingana na kundi la waasi la Sudan Liberation Movement/Army.
Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi siku ya Jumapili, huku aliyenusurika akiwa mtu mmoja tu wakati sehemu nyingi za kijiji cha Tarasin zikishuhudia "maafa" makubwa, kundi hilo lilisema katika taarifa.
Kundi hilo limeomba msaada wa kibinadamu kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa.
Wakazi wengi katika jimbo la Darfur Kaskazini walikuwa wametafuta hifadhi katika eneo la Milima ya Marra, baada ya vita kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) kuwalazimisha kuondoka makwao.