Inagusa sana: "Mwambie anipigie ni Mimi Mama yake"

Inagusa sana: "Mwambie anipigie ni Mimi Mama yake"

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Copy na ku-paste, Mimi sio mwandishi

Mwambie anipigie ni mimi mama yake! Mwambie sina simu ila nimeona picha zake kwenye simu ya kupalaza ya khamisi/mwambie amenenepa sana.

Mwambie nimeona gari lake ni zuri sana !!ila mwambie mama yake bado naishi kwenye lile banda pamoja na kuku/mwambie nimeumwa sana ila nikapona bila hata kutumia dawa/mwambie mzee juma bado ananidai pesa zake nilizokopa ili nimlipie ada amechukua kile kishamba nilichokuwa nakitegemea kufidia deni lake.

Mwambie mimi mama yake nimebaki pekee yangu tangu baba yake afariki sina hata wa kunisogezea kuni motoni.

Mwambie leo nimetamani sana nyama😭 zile mboga zilizoota zenyewe upenuni zimenichosha mpka mdomo umekuwa mchungu.

Mwambie wale vijana walitaka wanipige eti mimi mchawi eeh.

Mwambie mama yake nimekuwa mzee sana nahesabu siku tu aje hata nishike mikono yake nimuoneshe mipaka ya nyumba yetu.

Salio limeisha mwambie mama anampenda sana😭!ila huku kijijini nimebaki pekee yangu wenzangu wote wameenda mjini kusherekea kwa watoto wao...😢😢😢
IMG-20221226-WA0028.jpg
 
Watoto ndo huenda kusherehekea kijijini kwa wazazi wao, na sio wazazi kwenda mjini kwa watoto wao…. acheni kutia huruma kwa lawama zisizo na msingi.
 
MAMA AMLILIA MWANAE.jpg


Mwambie anipigie ni mimi mama yake!!mwambie sina simu ila nimeona picha zake kwenye simu ya kupalaza ya khamisi/mwambie amenenepa sana ..mwambie nimeona gari lake ni zuri sana !!ila mwambie mama yake bado naishi kwenye lile banda pamoja na kuku/mwambie nimeumwa sana ila nikapona bila hata kutumia dawa/mwambie mzee juma bado ananidai pesa zake nilizokopa ili nimlipie ada amechukua kile kishamba nilichokuwa nakitegemea kufidia deni lake/mwambie mimi mama yake nimebaki pekee yangu tangu baba yake afariki sina hata wa kunisogezea kuni motoni/mwambie leo nimetamani sana nyama
😭
zile mboga zilizoota zenyewe upenuni zimenichosha mpka mdomo umekuwa mchungu/mwambie wale vijana walitaka wanipige eti mimi mchawi eeh/mwambie mama yake nimekuwa mzee sana nahesabu siku tu aje hata nishike mikono yake nimuoneshe mipaka ya nyumba yetu/!!salio limeisha mwambie mama anampenda sana
😭
!ila huku kijijini nimebaki pekee yangu wenzangu wote wameenda mjini kusherekea kwa watoto wao...

Tuwatunze wazazi wetu jaman
 
Ni jambo lililo bora sana kulifanya, hapa duniani na ahera.

Japo kwa sie tulio wazazi wa leo tuwafunze wanenu kwa vitendo.

Ukipiga simu kwa mzee then mpatie wajukuu aongee nao, pia wapeleke wakamtembelee, wabebeshe zawadi kwa matumizi ya wazazi.

Kesho nao wakikuwa watajua kuwa kujali wazazi ndio namna ya kuishi.
 
Nmesoma kwa huzuni, tuwapende na kuwajali wazazi wetu. Kuna msanii fulani wa kibongo mdogo wake alinieleza jinsi alivyowatupa na kutowathamini wazazi wake nilijisikia vibaya mno, imagine hana mda wa kuwatafuta wazazi kuwajulia hali(hata kama ni ubize ndio miezi ipite na daily anashinda IG), Wazazi wakimtafuta anapokea na kuomba kuwapigia baadae yupo busy anakata simu na hapigi.
Tuwaheshimu sana wazazi ni baraka ya pekee
 
Back
Top Bottom