Pre GE2025 Inahitaji akili kubwa kiasi gani kuelewa kwamba kwa kuwa Zanzibar wana serikali na Rais wao, Rais wa Tanzania, kimsingi, ni Rais wa bara?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna nyuzi zingine ukiamua kukomenti ni sawa na kujisogezea kesi na kiziwi tu...😑
Halafu nyuzi za hivyo wenyewe wanakuwa wabishi kama mshipa.

Unamsoma halafu unasema eti huyu naye kajiona ana hoja kaandika post ndeefu imejaa ujinga na hata historia fupi tu ya 1985 imesahaukiwa.

Nikichogundua ni kwamba, Watanzania wengi hawampendi Samia (na mimi siko hapa kumtetea) ila katika kumponda wanatoa hoja za uongo na ukweli.

Hiki linasikitisha sana, kwa sababu Samia ana mapungufu mengi, hahitaji kutungiwa mapungufu mengine ya uongo.Ukintungia mapungufu mengine ya kufijirika, unakuwa sawa na mtu tajiri sana mwenye oesa nyingi ambaye hahitaji mkopo, lakini anaenda benki kuchukua mkopo wa riba kubwa sana ili kupata hela. Ujinga.

Ndipo hapo utasikia hoja za kuwa Samia si rais halali kwa sababu hajachagukiwa urais (zinazoonesha huyu mtu hajui katiba, hajui kuwa unapochagua rais unachagua a ticket, not a person) na hoja kama hizi ambazo hazitenganushi abstract thought na individual's problems, hazielewi au zinadharau muundo wa serikali ya Tanzania kikatiba, na kiujumla zina ujinga mwingi tu.

Kwa hivyo, nakuelewa sana.

Unaweza kusoma thread ukaona ujinga mwingi mpaka ushindwe pa kuanzia wapi.

Let's deal with facts. Samia kaharibu hiki na hiki na hiki.

Sio matatizo imagined kwamba hakuna Mzanzibari anayeweza kuwa fair akiwa rais wa Tanzania.

What does that mean, watu wa bara tu ndio wanaweza kuwa fair? Zanzibar si sehemu ya Muungano?
 
Kwenye maelezo hapo neno "Zanzibar" limefuata nini Sasa?
Mkuu, mimi siko extreme katika utumiaji wa haya maneno Tanzania bara, Tanzania visiwani, Zanzibar na Tanganyika. Nayatumia interchangeably, kwa sababu jina sio jambo kuu katika suala la mandhali ya muungano wetu. Tunaweza hata kuuvunja nikapendekeza ili kutoharibu brand ya nchi, Tanzania bara tuendelee kujiita Tanzania badala ya kurudi kwenye jina Tanganyika
 
Sijui kama nakuelewa. Sasa hapa Mkuu ndio tuseme unaona umetoa point kali ukilinganisha na issue zilizokuwa raised kwenye thread hii, ambazo sijui ndio unaita ujinga? Kama huu ndio mtazamo wako basi unachekesha sana 😀😀😀😀
 
Zamani kati hapa miaka ya 90s na early 2000s... nchi hizi mbili zilikuwa zinatambulika kama Tanzania bara na Tanzania Visiwani.

Sijui ilibadilikaje hii ID.
ILA UMEANDIKA UKWELI KABISA
 
Tuache masihara mkuu 'Synthesizer' ..."...marais kwa ajili ya upendo kwa nchi zao."! Kuna alama ya aina yoyote ambayo Samia alikwisha ionyesha katika utawala wake inayo kupa matumaini juu ya sifa hii yeye kuwa nayo kwa Tanganyika?

Katika mada yako ume yaeleza mengi ambayo sioni yanayo mhusisha na upendo kwa hii Tanganyika. Kiufupi ni kwamba, Samia yupo kwenye nafasi ya urais kwa sifa na maslahi yanayo patikana kwa kuwepo katika nafasi hiyo; basi.
Na kama ulivyo eleza vizuri kwenye mada, wanao faidika na uwepo wake kwenye nafasi hiyo ndio, ndiyo maana wako tayari kufanya kila liwezekanalo aendelee kuwepo hapo, hata ikilazimu kumwaga damu za waTanganyika.
 
Halafu nyuzi za hivyo wenyewe wanakuwa wabishi kama mshipa.
Ngoja nikujibu

Unamsoma halafu unasema eti huyu naye kajiona ana hoja kaandika post ndeefu imejaa ujinga na hata historia fupi tu ya 1985 imesahaukiwa.
  • Hueleweki. Inaonekana ni mzito au mvivu kusoma. Unapenda thread fupi. Umewahi kusoma kitabu kikubwa zaidi ya hadithi?
Nikichogundua ni kwamba, Watanzania wengi hawampendi Samia (na mimi siko hapa kumtetea) ila katika kumponda wanatoa hoja za uongo na ukweli. Hiki linasikitisha sana, kwa sababu Samia ana mapungufu mengi, hahitaji kutungiwa mapungufu mengine ya uongo.
  • Uongo na kweli, sawa. Na unakiri Samia ana mapungufu mengi, sasa kwa nini unalalamikia watu wanapomuandika sana juu yake? Hoja za namna hiyo zinapotolewa utaonekana kuwa na akili ikiwa utajibu thread kwa kusema upi ni uongo na upi ni ukweli. Sio kusema watu wanatoa hoja za uongo na kweli bila wewe kuisaidia jamii upi ni uongo na upi ni ukweli
Ukinitungia mapungufu mengine ya kufijirika, unakuwa sawa na mtu tajiri sana mwenye oesa nyingi ambaye hahitaji mkopo, lakini anaenda benki kuchukua mkopo wa riba kubwa sana ili kupata hela. Ujinga.
  • Huu mfano wako unafikirisha sana juu ya uwezo wako wa kupembua mambo. Kuna ubaya gani tajiri kukopa ili atumie hela ya benki kama atatengeneza hela zaidi? Mtaalamu yeyote wa biashara atashangaa sana kusikia unaita tajiri kukopa ni ujinga. Suala sio riba kubwa, bali ni kama mkopo utaingiza faida. Matajiri wanakopa sana, na ni kawaida katika biashara
Ndipo hapo utasikia hoja za kuwa Samia si rais halali kwa sababu hajachagukiwa urais (zinazoonesha huyu mtu hajui katiba, hajui kuwa unapochagua rais unachagua a ticket, not a person) na hoja kama hizi ambazo hazitenganushi abstract thought na individual's problems, hazielewi au zinadharau muundo wa serikali ya Tanzania kikatiba, na kiujumla zina ujinga mwingi tu.
  • Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu anaongea Samia sio raisi halali. Hili umelitoa wapi? Hapa nahisi wewe ndio unatunga hoja za uongo
Unaweza kusoma thread ukaona ujinga mwingi mpaka ushindwe pa kuanzia wapi.
  • Acha uvivu wa kusoma na kuishia kusoma vichwa vya thread kisha kutoa comment. Kichwa cha thread hakijasema Samia si raisi halali, bali raisi wa Tanzania ni raisi wa bara, na ukisoma thread utaona hakuna ambapo tumesema kwa hiyo raisi Samia sio rahisi halali
Let's deal with facts. Samia kaharibu hiki na hiki na hiki.
  • Sio lengo la thread hii. Thread hii imejikita kwenye suala la raisi toka Zanzibar kuwa raisi wa Tanzania katika mazingira ya muungano tuliyo nayo, ambayo yanamfanya raisi wa Tanzania kuwa raisi wa bara
Sio matatizo imagined kwamba hakuna Mzanzibari anayeweza kuwa fair akiwa rais wa Tanzania.
  • Anaweza kuwapo. Na hata tunaweza kuwa na Mkenya akawa raisi fair wa Tanzania. Lakini ni sahihi kufanya hivyo? Obama akiwa raisi wa Kenya atakuwa vizuri sana, very fair. Sasa kuna siku Obama atakuwa raisi wa Kenya? Elewa issue, usikurupuke kujibu
What does that mean, watu wa bara tu ndio wanaweza kuwa fair? Zanzibar si sehemu ya Muungano?
  • Hapana, anaweza kuwepo mtu wa bara kama raisi wa Tanzania akawa far worse kuliko Samia. Lakini sasa atakuwa ni wa bara akiongoza watu wa bara. Na Zanzibar ni sehemu ya muungano na ndio maana tunasema katika mfumo wa muungano tulio nao mtu wa Zanzibar hapaswi kuwa raisi wa Tanzania, kama ambavyo mtu wa bara haikubaliki akawe raisi wa Zanzibar
Kwa ujumla, nimegundua kwamba huna elimu ya kutosha kuelewa mijadala kama hii. Kama vitu huelewi sio lazima uchangie, hata kama JF inatoa uhuru wa kila mtu kuchangia thread
 
Zamani kati hapa miaka ya 90s na early 2000s... nchi hizi mbili zilikuwa zinatambulika kama Tanzania bara na Tanzania Visiwani.

Sijui ilibadilikaje hii ID.
ILA UMEANDIKA UKWELI KABISA
Ukitaka kufuatilia hilo limeshika kasi lini, hutakosa kuona alama zote zinazo mhusu Samia ndani yake, wakati akiwa Makamu wa Rais, aliye yeyusha "Kero" zilizokuwa hazina kikomo kabla yake.

Kama ni "Uzalendo" Samia ni MZALENDO mkuu wa nchi ya Zanzibar. Na ni makosa makubwa kuwa na Rais kwenye nchi nyingine ambayo hana 'uzalendo' nayo hata kidogo.
 
Sijui kama nakuelewa. Sasa hapa Mkuu ndio tuseme unaona umetoa point kali ukilinganisha na issue zilizokuwa raised kwenye thread hii, ambazo sijui ndio unaita ujinga? Kama huu ndio mtazamo wako basi unachekesha sana 😀😀😀😀
Kimsingi unasema hakuna Mzanzibari anayeweza kuwa fair kwa Jamhuri ya Muungano kote, atapendelea zaidi Zanzibar.

This is a value judgement on all Zanzibaris.

You have made the following logical fallacies.

1. Hasty generalization fallacy. Ume generqlize character za Wazanzibari wote bila ya kuwajua wote au kueleza logically tgat this observation is baswd on sonething innately Zanzibari.

2. Fallacy of composition. Bqsically saying that what is true of tge part is true of tge whole. Ukukutana na Mluguru kavaa shati jekundu basi unafijiri Waluguru wote wanavaa mashati mekundu.

Pia, uneweka bias ya Utanganyika. Kama unafikiri Mzanzibari hawezi kuwa fair kwa bara, kwa nini huoni tatizo hilo hilo kwa mtu wa bara kuwa fair kwa Qazanzibari?

Zaidi, umejitoa akili kwenye kuelewa muundo wa sasa wa Muungano, as bad as it is, lakini unatuongoza kuwa rais wa Muungano ni rais wa nchi nzima, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajiongoza katika mambo yasiyo ya Muungano tu, kama rais wa Muungano anamchagua gavana wa BOT, ambaye ni mmoja tu nchi nzima, gavana huyo ndiye anaongoza BOT mpaka Zanzibar.

Sasa hapo utasemaje rais wa Muungano ni wa bara tu?

Unaelewa katiba na mambo ya muungano ni yapi?

Hao mabalozi na mawaziri anaiwateua rais wa muungano ni wa bara tu?

Kwa nini unaweka vitu vya kujitungia wakati mambo yako wazi katika katiba?
 
First things first, rais wa muungano ni wa Tanzania nzima. Zanzibar ina mambo yake yasiyo ya Muungano inayojiongoza kwa hayo, mambo mengine kama ya fedha, mambo ya nje, etc, ni mambo ya muungano na Zanzibar haiwezi kujiongoza.

Ndiyo maana Salmin Amour alipotaka Zanzibar kujiingiza OIC alizuiliwa na serikali ya muungano.

Sasa hapo utasemaje rais wa muungano ni wa bara tu?

Hebu yasome mambo 22 ya muungano ambayo serikai ya mapinduzi ya Zanzibar haiwezi kujiamulia yenyewe.

PDF attached.

Pia tulishayajadili JF.

 

Attachments

Hakuna sehemu nimesema hivyo, kwamba hakuna Mzanzibari anayeweza kuwa fair kwa Jamhuri ya Muungano. Issue ni kwamba katika aina ya muungano sio jambo jema kujiweka katika hali hiyo. Tunaweza kuwa na raisi wa Zanzibar akawa vizuri kuliko hata raisi kutoka bara. Kwa mfano Dr. Omar Juma, huyu angekuwa raisi bora wa Tanzania kuliko hata Mkapa.

Ningeweza kusema hata Raisi Mwinyi wa sasa kuke Zanzibar, angekuwa raisi bora sana wa Tanzania - lakini waswahili wa Zanzibar watasema ni kwa sababu asili yake ni bara. Kwa hiyo hatuendi huko.

Labda nikuulize, wewe unaonaje, unafikiri raisi wa kutoka bara hawezi kuwa raisi fair akiwa raisi wa Zanzibar? Sasa kwa nini tusijaribu. Wote si Watanzania bwana.
 
Unatoka nje ya mada. Elewa thene ya thread. Mlifauluje mitihani yetu, Faiza Foxy hywa anauliza
 
Ninasubiri Professor Kabudi atoe ufafanuzi WA jambo hili.
 
Hapana.
Zanzibar ina maana kubwa sana kwa waZanzibari sasa hivi kuliko ilivyo wahi kuwa wakati wowote ule. Kwa hiyo, kama unafunika akili zako ili usilione hili utakuwa siyo mkweli kwa nafsi yako.

Mada yako imekuwa na dosari tokea mwanzo ulipo iwasilisha kana kwamba muungano ulio kuwepo 1985, ndio huo huo unao endelea leo hii; wakati hali ni tofauti kabisa.
 
Kwa mantiki hiyo, Samia ni mzanzibar ambaye amepata urais kuiongoza bara TU, ambayo kwa lugha za wasomi wenye PhD, waita Tanzania.
 
Currently Bara kunaongozwa na Mtaalamu kutoka nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…