Huu ni mtazamo mkuu! na inawezekana ulipata gari ikiwa tayali inamatatizo. Mimi nina Passo kwasasa mbali na nyingine ninazotumia, na nimekuwa nikienda karibu mara mbili kila mwezi Mwanza - Dodoma bila kuhisi hiyo shida ya kuchemsha.
Unaweza kuangalia yafuatayo:
1. Hakikisha rejeta yako imefanyiwa ukaguzi/kusafishwa na mtu ambaye ni mtaalam.
2. Jaribu kuachana na kuweka maji ya Duwasa/Dawasco au kisima kwenye rejeta - jitahidi kutumia coolant. Napendekeza utumie coolant bora sio zile zinazouzwa gerezani. Pata kutoka BP au kampuni nyingine zinazojitambua.
3. Fanya wholesome wngine check - ipimwe system yote. Garage za veta au kwengineko wanaweza kupima gari gako na kukushauri vipuri ambavyo tayali vimechakaa na unahitaji kubadilisha.
Naamini ukifanya haya mkuu wangu, tatizo linaweza kupungua.
TATIZO LA PASSO:
Gari nyingi aina ya Passo zona shida ya usukani kuwa mgumu - kuna indicator moja inajitokeza unapowasha gari "EPS" - ikitokea hiyo unaweza kushawishika kutupa gari kwani hata baadhi ya mafindi wa toyota hasa mikoani hawajui namna ya kurekebisha.
Zaidi ya shida hii sijaona. Kinachonifurahisha zaidi ni kuwa natumia 120,000/- mwezi mzima tofauti na gari zangu nyingine nilipokuwa natumia zaidi ya 250,000/- kwa mwezi (hii nazungumzia Mwanza).
Jitahidi matunzo kwa gari yoyote - utaipenda