Inahitaji ujasiri kununua gari kama hii

fredo fred

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
748
Reaction score
1,615
Hii ni starlet ya 1993 kwa hizi awamu ya tano kununua hii gari ni kama kufunga nayo ndoa.

Imagine hiyo starlet hapo chini ina usajiri wa DQR na anaiuza 6M sasa kwa usawa huu kweli kwenda kununua gari kama hiyo naona ni kupoteza pesa tu ni bora kununua vitz au starlet ya model kuanzia 1996 aubgari nyingine yoyote ambayo model yake atleast ni ya mwaka 2000.

Kumpata mtu wa kununua hiyo gari ni kazi kubwa ukizingatia gari yenyewe ni manual transmission.

Hio gari inayouzwa used 6m ina AC na power steering tu haina power windows yenyewe ni kutumia handle tu

Mtizamo wangu unaweza kuwa + au -View attachment 1678721View attachment 1678724View attachment 1678723View attachment 1678722View attachment 1678726View attachment 1678725
 
Kigari kigumu sana hicho na ni manual ...manual ina raha zake asikwambie mtu..halafu wese kijiko...
 
Ninayo moja ambayo ni Starlet gt turbo ep 82 ni safi sana ndugu mtoa mada, nimekuwa na gari tofauti kama vile Cresta Gx 100, Mark 11 grand, vitz, Carina nk lakini zimeikuta na zimeondoka na hiyo ipo pale pale.
 
Ninayo moja ambayo ni Starlet gt turbo ep 82 ni safi sana ndugu mtoa mada, nimekuwa na gari tofauti kama vile Cresta Gx 100, Mark 11 grand, vitz, Carina nk lakini zimeikuta na zimeondoka na hiyo ipo pale pale.
Upo sahihi ila kuiuza hiyo gari kwa sasa itakuwa shida na kama ina namba A unaweza kujikuta unaiuza hata kwa 1.5m
 
Kigari kigumu sana hicho na ni manual ...manual ina raha zake asikwambie mtu..halafu wese kijiko...
Kuna gari nyingi tu ni ngumu za kuanzia mwaka 2000, pia usinunue gari kwa ajili yako tu, kuna siku isiyo na jina unaweza pata shida ukataka hiyo gari uiuze ikisaidie kutatua shida yako.

Sasa kwa gari ya zamani kama hii umenunua kwa gharama kuubwa halafu ukitaka kuiuza wateja wanapatikana kwa shida, na hata akipatikana atataka umuuzie bei ndogo sana (robo ya bei uliyoinunulia ww)

Labda kama ww ni tajiri sana ndo unaweza kununu gari hata zile zisizouzika kirahisi, kwa maana utakuwa na njia nyingi za kutatua shida zako.

Ila kama maisha yako ni ya kawaida tuu.....nunua gari ambayo hata ukitaka kuiuza haikuchukui muda mrefu.
 
Kweli kabisa mkuu
Kununua gari kama hiyo kwa kipindi hiki ni upotevu wa hela nje nje kabisa maana hiyo gari hapo sidhani kama ataweza kuuza kwa bei aliyoiweka
 
Mkuu imekukosea nini starlet ya watu, mbona umetumia nguvu nyingi sana kuikosoa?
Haijakosea starlet....bali aliyekosea ni aliyenunua hyo starlet ya miaka 29 iliyopita halafu anataka kuiuza bei ambayo hata ist ya mkonon na gar nyingi tu za kuanzia mwaka 2000 unapata.

Maana hicho kigari hata usalama wake ni mdogo sana kulinganisha na matoleo ya kuanzia mwaka 2000 na kuendelea.
 
Bora umeliona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…