Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Sio kila jambo ni la kushea,binadamu tuna marafiki,wazazi na ndugu,wote hawa kila kukicha tunasema tunawapenda lakini linapokuja suala la mapenzi hapo tunataka tuwe wenyewe tu. Japokua zipo imani na mila zinaruhusu mahusiano ya kindoa kuwa na mke zaidi ya mmoja maumbile bado yanakua kinyume na ruksa hii, yanasimama peke yake, mwanadamu hataki kuwa na penzi la kushea na mwanadamu mwenzake.Lakini pia katika mahali ambapo mwanadamu anaonekana mnafki na mwenye choyo ni eneo hili.
Ni mnafiki kwa sababu mwenzi wake anataka awe wake yeye tu lakini yeye akitaka awe na mahusiano mengi.Jambo hili ni kwa jinsia zote.Lakini pamoja na kuwa na mahusiano na wapenzi wengi bado mwanadamu hatosheki, ruhusa ya kuwa na wake wa 4 imeshindwa kumsaidia mwanaume, "maendeleo" ya kuanza ngono kwa idadi ya wapenzi unaotaka ukitosheka ufunge ndoa nayo imeshindikana,sasa zimekuja ndoa za mikataba unaweza kuoa/kuolewa leo na ndoa ya mkataba wa wiki moja baada ya hapo unakua huru.
Mwanadamu hana tofauti na mbuzi ambae anampanda mama yake!Mi napata wasiwasi kama huyu mwanadamu ndo yule alieumbwa mwenye mfano wa Mungu.Mi nadhani ni wakati muafaka wa kujiuliza,hivi wanawake wote au wanaume wote niliofanya nao ngono nimefaidika na nini?Je huu ni ubinadamu kweli?
..Kama kweli tunataka furaha ya kweli tuache unafiki na tujitazame bila kujipendelea kisha tubadilike.Kuna watu wameshafanya ngono na wanaume au wanawake ukiwakusanya wanajaa basi nne.Ukimuangalia alichopata cha maana hakuna zaidi ya umaskini mkubwa!