Inakuaje Mchina Kariakoo anauza bidhaa/vitu kwa bei chee lakini Mtanzania anakuuzia kwa bei ghali? Kwanini Mtanzania naye asiuze bei chee kama Mchina?

Inakuaje Mchina Kariakoo anauza bidhaa/vitu kwa bei chee lakini Mtanzania anakuuzia kwa bei ghali? Kwanini Mtanzania naye asiuze bei chee kama Mchina?

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,139
Reaction score
2,223
Inakuaje Mchina Kariakoo anauza bidhaa/vitu kwa bei chee lakini mtanzania anakuuzia kwa bei ghali? Kwanini mtanzania naye asiuze bei chee kama mchina?

Mfano unakuta mtanzania anakuuzia kitu kwa 90,000/= Tsh lakini ukienda kwa mchina anakuuzia 45,000/=Tsh

Kwanini mtanzania asiende kununua kwenye bei chee kwa mchina kuliko kununua bei ghali kwa mtanzania mwenzake.

Kama mzigo wote wanafata sehemu moja kwanini gharama ziwe juu.

Tatizo nini? Sera za wawekezaji? Au kuna mikataba ya siri ilisainiwa kuwapa upendeleo wa China?

(Mdau anauliza mtaani)

Ufafanuzi tafadhali yakinifu wataalamu karibuni

Screenshot_20240623-134117.png
 
Kwanza ungejiuliza hivyo vitu vya Mchina vinatoka Nchi gani? Ukishapata jibu fanya tafakuri utaelewa?
Vinatoka China, wote wanafata china au hao wachina wanaletewa bure? Au hapo bandarini hawalipii kodi.?

Maana hata hawa wafanyabishara wa KARIAKOO wanatoa mizigo zao China huko huko wanalichukulia hawa wachina.

Au Nchi ya China inawapa kipaumbele wananchi wake kwa kuwapa mikopo nafuu yenye riba nafuu.?

Kuliko wafanyabishara wa Tanzania kwa nchi yao?

Ndio maana tupo hapa kuelimishana wengine sio wabobevu katika masuala ya biashara

Nipo tayari kuelekezwa
 
Kwanza ungejiuliza hivyo vitu vya Mchina vinatoka Nchi gani? Ukishapata jibu fanya tafakuri utaelewa?
Bidhaa nyingi wanazouza wabongo na wachina zinatoka nchi moja, China! Inafikirisha bidhaa iliyo kwa mchina unaipata bidhaa hiyo hiyo kwa mbongo kwa bei mara mbili zaidi!

Halafu ukienda duka la mchina ukikutana na winga kama huelewi, lazima atakupiga bei mara mbili pia, maana wanakuwaga mbele ya maduka yao wanavizia wageni!

Winga atakuambia bidhaa 12,000/= na anakuzuia usiende direct kwa mchina, maana anajua hiyo bidhaa utaipata kwa 6k au chini ya hapo!
 
Wachina wengi ni wazalishaji bidhaa na huuza kwa jumla. Bei ya jumla ni rahisi lakini lazima mnunuzi ununue mzigo mkubwa.

Wabongo wanauza bei tofauti kwa sababu wengi wanauza jumla na rejareja. Uwezi ukauziwa bidhaa let say kiatu pair moja kwa bei ya jumla, faida ataipata wapi?
 
Wabongo wangapi wana viwanda china? Industrilization kule walianza kitambo...kuachana na hivyo tu..sheria zao ni kali sana tukianzia kwa kiongozi wao wa mwanzo Mao Tse Tung, huyu mwamba aliamin katika uwajibikaji wakufanya kaz kwa bidii na aliwaua wachina wengi sana ambao walikuwa wavivu.

China skilled lbrs ni wengi haswa tena wenye umri mdogo haswa...na wana bidii kwenye kazi..sio wavivu na sio china tu, nenda south/ North korea wapo hivyo, ingawa kwa wabongo kufanya shughuli kwenye hizo nchi na wakatoboa ni kaz kubwa sana, lakin wenyewe wakija huku miez mitatu mingi..kwanza hata ku adopt lugha ya kiswahili ni wepesi sana kwa kifupi wapo seriouz na wafanyacho.

Labda nikupe mfano mmoja, mo anafanya production ya vitenge na kiwanda kipo lakin hawez kidhi mahitaji, demand ni kubwa kuliko production yake..na hata bei yake ni kubwa hatuna uhakika wa umeme Tz kwa hyo costs za productions lazima ziwe juu.
 
Bidhaa nyingi wanazouza wabongo na wachina zinatoka nchi moja, China! Inafikirisha bidhaa iliyo kwa mchina unaipata bidhaa hiyo hiyo kwa mbongo kwa bei mara mbili zaidi!
Halafu ukienda duka la mchina ukikutana na winga kama huelewi, lazima atakupiga bei mara mbili pia, maana wanakuwaga mbele ya maduka yao wanavizia wageni!
Winga atakuambia bidhaa 12,000/= na anakuzuia usiende direct kwa mchina, maana anajua hiyo bidhaa utaipata kwa 6k au chini ya hapo!
Kuna haja ya kuyafahamu maduka ya wachina ili mtu uwe unaenda moja kwa moja hata kama mawinga watakuzuia utaweza kuwapita tu.
 
Kuna haja ya kuyafahamu maduka ya wachina ili mtu uwe unaenda moja kwa moja hata kama mawinga watakuzuia utaweza kuwapita tu.
Kwa wanaoyafahamu mawinga hawawasumbui, wageni wasio na wenyeji ndio wanadakwa kirahisi na mawinga, ila ndio hivyo akishadakwa mara moja kama mjanja muda mwingine anakwenda direct kwa mchina!
 
Kwa wanaoyafahamu mawinga hawawasumbui, wageni wasio na wenyeji ndio wanadakwa kirahisi na mawinga, ila ndio hivyo akishadakwa mara moja kama mjanja muda mwingine anakwenda direct kwa mchina!
Siku zote lazima tuanzie kwenye practice then ndio tuujue mchezo, sio mbaya kwa mara ya kwanza ukidakwa na mawinga. ila ukiwa na mwenyeji(muaminifu) ndio inakuwa poa
 
Back
Top Bottom