Inakuaje watu huwa wapo tayari kuchangia harusi na Msiba ila sio pale mgonjwa anapoumwa

Inakuaje watu huwa wapo tayari kuchangia harusi na Msiba ila sio pale mgonjwa anapoumwa

harusi na misiba ni malipo ya mara moja, imeisha hio na kuna uhakika mkubwa wa sherehe / mazishi

Kuuguza mgonjwa ni malipo ya mara kwa mara na hakuna uhakika atapona, hapa kuna watu wanaweza kukusaidia mwanzoni ila kuna muda inafika wanatokomea, kwasababu mgonjwa anakuwa mzigo kiuchumi (Sipendi kuyasema haya lakini ndio sababu)

Leo mchango wa dawa, kesho unapigiwa simu mchango wa vipimo, hujakaa sawa utatafutwa uchangie gharama za upasuaji, unatafutwa tena mchango wa gharama za kulazwa, baada ya muda unatafutwa mchango wa gharama za vifaa, baada ya hapo unatafutwa uchagie safari ya Nairobi, n.k.

CONSLUSION: Watu wanapenda kulipia vitu mara moja vyenye uhakika, Hawapendi kuchangia mara kwa mara na hakuna uhakika , nje ya matibabu kuna ada za shule (hakuna uhakika wa ajira),
 
tanzania na watu wake wamekata tamaa ya maisha ndio maana wana vikundi vingi vya kufa na kuzikana hawajawai kuwaza kuanzisha vikundi vya kusaidiana kimaendeleo
Inasikitisha sana
 
Mleta mada me naomba niongezee hapo tu sio ugonjwa tu hata Ada unakuta mtu kakosa mkopo wa chuo tena course ya udaktari na wanaukoo wanajua ila wanajikausha.
 
Mleta mada me naomba niongezee hapo tu sio ugonjwa tu hata Ada unakuta mtu kakosa mkopo wa chuo tena course ya udaktari na wanaukoo wanajua ila wanajikausha.


MTU anaacha chuo kisa kakosa Mil 2 Ila akisema anaoa au kuolewa atachangiwa zaidi ya hiyo hela .

Mentality
 
Ila watu wasilaumiwe moja Kwa moja, yaani mtu kweli anaweza haña pesa kabisa ila siku msiba unatokea hata amdeni wako ambaye umesahau anakuja kulipa, hivi unaijua pesa wewe, (hujasikia kuwa pesa shetani)
 
Wabongo mmezidi michango, kila kitu mchango
Mimi nimefukuzwa magrupu kibao kwa kuamua kujikausha
😀😀
Hii imenifurahisha na kunihuzunisha ,juzi nilikuwa added kwenye group la kazini bila kuomba ila group linahusu harusi ya workmate ,waliposema na Mimi ni mwanakamati ,nikasema siwezi na hela Sina ya kutoa .
Ndani ya dakika mbili niliondolewa katika group ,nikacheka nikasema hawa tutakutana asubuhi waniambie kwanini kunifanyia hivyo .

Eti asubuhi nawaona wahusika kila mtu kajinunisha nikasema saaaafi kabisa mpaka kidume kujinunisha basi meseji imewafika .

Ila kwenye suala la shida Mimi nahimiza tuchangiane jamani ,hapa duniani sisi ni wageni tu
 
Dunia ya sasa watu wamekuwa wabinafisi ,huwa wanafanya kitu ambacho watanufaika nacho moja kwa moja.
Mtu anapo changa harusi ana jua kuwa atakula ,atakunywa,atacheza mziki, sasa ukimuchangia mgonjwa haunufaiki moja kwa moja.
Hivi kweli utamaduni huu wawezakuwa umetoka wapi?

Nakumbuka zamani mtu aliandaa harusi kivyake na akaalika watu, wakala na kunywa wakafurahi, mambo yakaisha namna hiyo.

Mtu hakuhitaji mchango wa mtu ili akamilishe jambo lake.
Lakini sasa hivi ni vurugu, na kwenye 'vyumba vya madhehebu' ndiyo usiseme, ni balaa.
 
Na mkiwa wazima muwe mnasalimia ndugu,jamaa na marafiki.
Kuna mtu akiugua ndiyo anakumbuka kuwa ana ndugu X

Ubinadamu kazi sana.
Hilo nalo neno, mtu akiwa vizuri hakumbuki chochote hata kujiwekeza hakuna ni kula tu bata, ila siku aliumwa anatafuta wale aliokuwa anawapuuzia wamsaidie uliona wapi hayo.
 
Back
Top Bottom