harusi na misiba ni malipo ya mara moja, imeisha hio na kuna uhakika mkubwa wa sherehe / mazishi
Kuuguza mgonjwa ni malipo ya mara kwa mara na hakuna uhakika atapona, hapa kuna watu wanaweza kukusaidia mwanzoni ila kuna muda inafika wanatokomea, kwasababu mgonjwa anakuwa mzigo kiuchumi (Sipendi kuyasema haya lakini ndio sababu)
Leo mchango wa dawa, kesho unapigiwa simu mchango wa vipimo, hujakaa sawa utatafutwa uchangie gharama za upasuaji, unatafutwa tena mchango wa gharama za kulazwa, baada ya muda unatafutwa mchango wa gharama za vifaa, baada ya hapo unatafutwa uchagie safari ya Nairobi, n.k.
CONSLUSION: Watu wanapenda kulipia vitu mara moja vyenye uhakika, Hawapendi kuchangia mara kwa mara na hakuna uhakika , nje ya matibabu kuna ada za shule (hakuna uhakika wa ajira),