Inakuwaje baadhi ya wanawake wapo tayari kumwacha mwanaume anayempenda kisa fedha baadaye anarudi na kutaka muwe wapenzi kisirisiri?

Inakuwaje baadhi ya wanawake wapo tayari kumwacha mwanaume anayempenda kisa fedha baadaye anarudi na kutaka muwe wapenzi kisirisiri?

kamba0719

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Posts
804
Reaction score
1,906
Nilisha simuliwa story hizi nyingi za mwanamke kumwacha ampendaye kisa kampata mwengine mwenye hela.

Nina wanangu wa wawili wote mainjinia, mmoja nilijuana naye Mchikichini kwenye mapindi, mwengine tulijuana kwenye projects moja ambayo ilikuwa tempo ya kama mwaka mmoja.

Huyu mwana niliyejuana naye kwenye mapindi Mchikichini, yy demu wake alianza naye tolea Secondary, mwana yupo A-Level na dem O level (kampita madarasa matatu).

Bahati nzuri mwana alivyo maliza chuo akapata kazi na demu naye akaingia chuo UD,mwana alikuwa anamsapoti demu zile hela za matumizi chuo.

Hee kumbe kule alipokuwa akifanya field kwa miaka miwili, akaanza mahusiano na jamaa mwengine ambaye yupo vizuri kiuchumi.

Demu anamaliza chuo, akatafutiwa kazi na yule jamaa mwana hajui, sasa nakumbuka kama sikosei 2016 au 15 mwana akatuambia mimi mwaka huu nataka kuoa, tukamwambia poa oa tutakupiga tafu, baada miezi mitatu demu katolewa mahali na kapewa mkoko wa kumtembelea, mwana anaambiwa na yule demu alichoka baada kama miezi 5 demu akaolewa.

Daah mwana alipungua hana raha mwaka mzima siku zikaenda kama baada ya mwaka na nusu baada ya ndoa,yule demu karudi kwa mwana eti wawe wapenzi kisirisiri mme wake asijue, mwamba kampiga stop kwamba asimsumbue still demu mpaka sasa bado anamsumbua mwana na mwana hana time nae.

Huyu pili yy demu walikuwa wana miaka miwili, demu alimaliza chuo ila hakuwa na issue mwamba alikuwa anapata projects hizi za miezi sita,mitatu, mwaka.

Nakumbuka 2017 kuna project tulipiga wote by mwezi wa 10 ,projects ikaisha tukaambiwa kuna nyingine ina sites kama 1600,ila Bahati mbaya ile tenda hawa kuipata.

Nakumbuka sasa 2018,mwana akawa anapitia msoto yule demu 2018 kapata kazi akawa anamletea dharau mwana, akitoka ofisini anarudishwa na mkoko mpaka home, baadae akaamua kumchana waachane kwani kapata mwengine.

Daah mwana alichoka sana kwanza stress za kuwa hana kazi pili za kuachwa na demu

Mwamba nae 2019 February anapata kazi mshahara 2.3m,mwana kidogo sasa yupo vizuri.Baada ya miezi kama 5 ya mwana kuanza kazi ,demu anarudi naye anamwomba mwana wawe wapenzi kisirisiri, daah kwanza mwana alimtukana,akampiga biti hasithubutu kumtafuta wala kumtafuta kwenye simu kwani ana mahusiano mapya.

Na hawa mabinti wote waume zao ni wana hela ndefu, kuliko hawa mwanangu kwani yule kwanza anakunja 1.9m na wa pili 2.3m ila leo kesho wanawasumbua wana.

Sasa na jiuliza inakuwaje unamwacha mtu unayempenda kwa dhati kisa fedha then kesho unaomba urudiane nae hivi huwa mnafikiria nini.
 
Ni kazi sana au ni kuendekeza umalaya? Huna hofu ya Mungu, mwenzio anapambana, kwa ajili yenu wawili kwanini usimuombee na umpe moyo no condition is permanent, misemo ya kipumbavu kama hio eti ni kazi sana, either wewe ni gold digger au unafanya biashara pendwa ya madada poa.
Brother jiheshimu..... Hofu ya Mungu ya unaijua ww....punguza kukurupuka.... Gold nyokwe unamjua ww shenzi

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Njaa na kuotokujua nini maana ya upendo na nini msingi wa ndoa,mbele ya pesa mwanamke huwaga anasahau kuangalia true love,ila akienda kule akikuta kile alicho kitarajia hakipo ndipo anapokumbuka fedha si kila kitu, upendo ni zaidi ya fedha, kwani ndani ya upendo kuna furaha na amani.

Ila yote tisa kumi ni yule mwanaume aliye muoa lazima atapitia hali ngumu sana.
 
Mkuu ilikua hivi..... Mim nliingia kweny mahusiano na mtu Hana pesa na me Sina...... Tukaweka mikakati ya kuzitafuta pesa kweli kila mtu anatoka kidg knachopatikana yanafanyika maendeleo..... Badae mambo yakawa SawA hapo sasa mwenzangu ndo akaanza marafik na kua mchepukaji mashuhuri..... Badae nkasema hapana nkaondoka nkaanza maisha yangu upya taratibu..... Mwanzo nlipata magum man sikua hata na kijiko...... Badae mambo yakakaa SawA.... Sa hv anataka turudiane...... Kwa hyo sio tu wanaume wanapitia hayo mambo hata wanawake pia..... Nmesema kumvumilia mwanaume ambae hana pesa ni wanawake wachache wenye uwezo huo kwa sabb me nmepitia maisha hayo!

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Hata mwanaume mwenye pesa ana maudhi yake ...
All in all mi nlichomaanisha Ni kuwa wanawake/wanaume wazuri WaPo wenye Hela Na wasio nazo
Pia wanawake/wanaume wabaya WaPo wenye Hela Na wasio nazo..
All in all pesa isiwe kigezo cha kumdefine mtu kwenye mahusiano...Maana Kuna wanawake wameolewa Na matajiri Na wanajuta Na Kuna ambao wameolewa Na masikini Na Wana furaha.
 
Alikuwa promote, nikajua we will still be on the same boat.. baada ya miezi sita,nikabwaga manyanga kiboba moja wa TRA alikuwa na hudumia.. three years later, she is ready to do anything to win my heart back, hta ka itakuwa nikuwa mke wa pili...and she's very serious wanawake bhana.
 
Back
Top Bottom