Inakuwaje binadamu ndio mweye akili lakini analipia gharama kuishi?

Inakuwaje binadamu ndio mweye akili lakini analipia gharama kuishi?

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Japo ndio kiumbe mwenye akili kuliko wenzake hapa Duniani.

Ila kwa maisha yake yote anagharamia.

Lazima, alipie maji, nyumba, umeme, mavazi, chakula, usafiri, matibabu , mapenzi n.k.

Yaani hata Konokono kamshinda maana ana nyumba yake na halipii kodi.
 
Kwasababu hiyo ni puzzle halisi iliyosolve puzzle fichi.
 
Tungeweza kuishi maporini na kula matunda pori, mizizi, majani na raw meat...

Lakini akili na maarifa yaliyofanya uvumbuzi wa vitu mbalimbali yanapaswa kugharamikiwa...
 
Kulipia huduma ni matakwa ya mtu binafsi,hakuna aliyemlazimisha mtu kulipia

1.Ukitaka usilipie Nyumba nenda porini fyatua tofali Jenga yako uishi Bure

2.Ukitaka usilipie umeme,Jitengenezee umeme au Jitengenezee Koroboi/Kibatari weka mafuta ya zeituni iwake uendelee na maisha

3.Ukitaka usilipie Maji nenda hapo kwako chimba kisima Kwa kutumia sululu na jembe ili uji mwayemwaye

4.Ukitaka usilipie usafiri tembea Kwa miguu au Tafuta punda ufuge,wengine uwafanye kama usafiri

5.Ukitaka usinunue Chakula,nenda porini fyeka vichaka lima mashamba yakupatie nafaka na mboga mboga

6.Ukitaka usinunue nguo,tengeneza shamba panda pamba na ujitengeneze nguo zako!

Ukifanya hayo hizo gharama zisizo za lazima utaziepuka!
 
Binadamu hana akili kabisa kila kitu Ana struggle kupata kila kitu.
Kabisa.
Nyani halimi. Tunalima sisi anakula.

Tunatenga mbuga, tunaweka wanyama tunaenda kuwaangalia wanyama wenzetu tunalipia.

Mtu akisikia njaa akiwinda swala ale anafungwa..

Tumewekeana mipaka tusivuke mwenda nchi nyingine lakini sisimizi na siafu wanavuka Bure.

Tumeharibu maisha yetu wenyewe.

Matayo 6:25

Neno: Bibilia Takatifu

Msiwe Na Wasiwasi​

25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi?

Matayo 6:26

Neno: Bibilia Takatifu

26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege?
 
Ni kweli mkuu. Tunahangaika kwakuwa tunauharibu mpango wa Mungu juu yetu.
 
Ni kweli mkuu. Tunahangaika kwakuwa tunauharibu mpango wa Mungu juu yetu.
Ukweli ni kwamba binadamu was not designed for foraging kabisa kabisa.

Hata ukiangalia muundo wa miili yetu ni milaini na Haina nguvu. Haikuumbwa hii miili ijitafutie bali Lengo lilikuwa tukae tulishwe kama mana jangwani vile sema ndio Adam na Eva wakazingua.

Angalia wanyama wengine wana kucha Kali, ngozi nzito, meno makali na macho yanaona mpaka kwenye Giza plus mbio za maana.
 
Back
Top Bottom