Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kati ya Mambo ambayo yatakuja kukiondoa Chama cha Mapinduzi madarakani ni namna ambavyo hawagawi kwa usawa keki ya taifa.
Siku Watanzania wakipata akili na kusema kwa nini hapa kwetu tunachangia hiki na hatupati hiki ndio utakuwa mwisho rasmi wa siasa za kutawala Tanzania kwa Chama cha Mapinduzi.
Nipo Jijini Dar es Salaam. Jiji linaloongoza kwa makusanyo ya kikodi pamoja na kuchangia zaidi katika pato la Taifa.
Kilichonisikitisha ni namna jiji hili lilivyo na barabara mbovu. Yaani ukisema unaenda Mbezi Msumi ni sawa na kusema naenda kuharibu gari yangu.
Ukisema unaenda Kigamboni barabara za mitaani hazifai. Sema uende Bungu sijui Mabwepande napo barabara za mitaani hazifai.
Ukija Mbezi Beach ambapo unasema wanakaa watu wenye uwezo napo barabara za hovyo hadi zinatia huruma. Nenda Tabata, Mbagala, Gongo la Mboto hali ni hiyo hiyo.
Swali nililojiuliza ni kwamba endapo hawa watu wakipata akili za kuhoji kama tunavyoona Gen Z ya Kenya chama changu CCM fungasheni virago haraka sana.