Inakuwaje Dar es Salaam inaoongoza kuingiza mapato ya Nchi unakuwa na barabara mbovu hivi?

Inakuwaje Dar es Salaam inaoongoza kuingiza mapato ya Nchi unakuwa na barabara mbovu hivi?

Masaki ndio aibu kabisa mpk unajiuliza huku sindio wanakaa mabaloz,matajir na viongoz haya mashimo hawayaon au Yan full mashimo na viraka
 
Masaki ndio aibu kabisa mpk unajiuliza huku sindio wanakaa mabaloz,matajir na viongoz haya mashimo hawayaon au Yan full mashimo na viraka
Inasikitisha. Ni kama Dar wameisahau.

Mbaya zaidi pesa za Dar zinaenda kuijenga Dodoma. Dodoma zinajengwa barabara za lami sehemu ambazo hazina hata watu!
 
Pato gani la mkulima linalizidi pato la Jiji la Dar es Salaam?

Nipe takwimu ya miaka hata 5 mfululizo mkoa unaaoongoza kwa kuliingizia taifa mapato makubwa uone kama kuna mkoa umeizidi Dar es Salaam?

Then ndo utaelewa hoja yangu hapa!
Screenshot_20240629_130917_Google.jpg

Ebu niambie, kati ya hivyo 👆 Dar mnalima na kuexport nini?
 
Kati ya Mambo ambayo yatakuja kukiondoa Chama cha Mapinduzi madarakani ni namna ambavyo hawagawi kwa usawa keki ya taifa.

Siku Watanzania wakipata akili na kusema kwa nini hapa kwetu tunachangia hiki na hatupati hiki ndio utakuwa mwisho rasmi wa siasa za kutawala Tanzania kwa Chama cha Mapinduzi.

Nipo Jijini Dar es Salaam. Jiji linaloongoza kwa makusanyo ya kikodi pamoja na kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Kilichonisikitisha ni namna jiji hili lilivyo na barabara mbovu. Yaani ukisema unaenda Mbezi Msumi ni sawa na kusema naenda kuharibu gari yangu.

Ukisema unaenda Kigamboni barabara za mitaani hazifai. Sema uende Bungu sijui Mabwepande napo barabara za mitaani hazifai.

Ukija Mbezi Beach ambapo unasema wanakaa watu wenye uwezo napo barabara za hovyo hadi zinatia huruma. Nenda Tabata, Mbagala, Gongo la Mboto hali ni hiyo hiyo.

Swali nililojiuliza ni kwamba endapo hawa watu wakipata akili za kuhoji kama tunavyoona Gen Z ya Kenya chama changu CCM fungasheni virago haraka sana.
Sema Keybord Worriour
 
Kwanza exports ndo zinazoongoza kwenye makusanyo yaliyopo TRA?

Uliza izo exports zimeingiza shs ngapi kwenye mfuko wa hazina alafu compare na makusanyo ya Jiji la Dar kwa mwaka wa fedha mmoja tu alafu rudi hapa
Kama hayo makusanyo ya madafu yenu mnaweza kuyatumia kununua mitambo ya kujengea barabara, then go ahead.
 
Kwanza exports ndo zinazoongoza kwenye makusanyo yaliyopo TRA?

Uliza izo exports zimeingiza shs ngapi kwenye mfuko wa hazina alafu compare na makusanyo ya Jiji la Dar kwa mwaka wa fedha mmoja tu alafu rudi hapa

View: https://youtu.be/pfunGatK8CM?feature=shared
Haya ndiyo mambo sisi wakulima tunaifanyia nchi wakati hata huduma zetu za kijamii ni za kubangaiza. Nyie mabishoo wa Dar kazi yenu ni kulalamika tu wakati mna barabara mpaka za ghorofa, na sisi tuna vinjia tu!
 
Hili kwa wasomi wetu mainjinia na waziri wa ujenzi hawatutendei haki wakazi wa dsm.
Tunahitaji service road karibu barabara zote , tunahitaji barabara ziwe pana ili magari yaweze kupishana kwa wingi.
Hili la mwendokasi naona kama ile ya kimara ilikiwa inatosha huku kweingine barabara zipanuliwe ziwe na lane 6 hadi 8 na watu binafsi waingize daladala za maana luxury coach na bei inakuwa premium. Ndio wenzetu wanavyofanya .
Moja ya sababu watu wengi wanamkumbuka magufuli ni ujenzi wa lami bora katika jiji na nchi. Kule mbweni kuna lami zimewekwa siku hizi ni kama yeboyebo hazina mwaka potholes kibao
 
Back
Top Bottom