Inakuwaje Mambo haya??

Never rush in love for it never runs out. Let love be the one to knock at your door, so by the time you start to fall, you know that your feeling is for sure.
 
NImesoma hii thread... na bahati mbaya sana sikuiona kabisa maana nilikua bize kweli na povu za siasa (dada regia kaniambukiza kabisa siku hizi)

Mdogo wangu MJ1
Binafsi naamini kwamba binadamu tupo tofauti kama ambavyo fingerprints zetu zilivyo... OSme of us live life ile ya high na low kama mawimbi ya bahari, na kama umeandikiwa hivyo basi ujue kwamba utakua hivyo hadi unaingia kubrini... Pole kama nawe ni mmoja wao. Ila kwa hili siamini wewe u-mmoja wao, wengi wa aina hii hutokana na kukosa confidence au kuwa na huruma zilizozidi... sometimes ni ile hali ya kutotosheka hasa ukilinganisha na previous love life... Kuna watu wamepewa roho ya huruma sana na usahaulifu usio na kifani, hao nao huumia na kuishi a very unstable life, AU UNA EGO YA KUKATAA KUTOSWA HADI UTOSE WEWE... HAVE EVER FELT BAD UKIMTOSA MTU? KAMA SIO BASI UJUE UNAPENDA KUSHINDANA NA MOYO WAKO

Sasa on your case... yawezekana unamiss replacement, you pick wrong types au you are just not sure of what you want to do... Hata tufanyeje, au tu advice nini... in the end wewe ndiyo mwenye moyo na pia mwenye mapenzi

ushauri wangu ni mmoja tu.... learn to lose, learn to give up, learn to be selfish and learn to be proud of your self and your decisions... YOU ARE GIVING TOO MUCH AWAY!!!

If I were you, I wouldnt ever give my heart to a person that I am sure of her capability to hurt me one more time!!
 

Kaka .......................where have you been ...........and who are you? Have we ever met?? mbona naogopa sasa.......... very unfortunately kuwa everything you have put down here its almost true.... ah.........
Hey but I have learnt my lessons kaka though in a hard way but my head is up now. Thanks and for sure I am taking this piece of advice with me.

Once again......thank you
 
Poleni nyote kwa yaliyowasibu ndo maisha popote utakapokimbilia.

Mimi nipo tayari kupendwa na kupendeka
 
Ni kweli haya mambo yanaumiza but tukimtanguliza Mungu hakuna kinachoharibika if he/she is made to be urs he will always be urs and if not it can happen hata ukimpa nini
 
MTM......imenibidi kuirudia post yako maana uliyoyaandika mwe...........sasa hapo pa kufall fro wrong types......Uwilll so we have types eh?? I thought mapenzi hayachagui na ukipenda unapenda?? Hebu tufundishane jamani kuidentify our types....tunapaswa kuangalia vitu gani??
 
Duh kaka lazima utakuwa senior citizen kama mimi...teh teh teh.....manake wengine tushazeeshwa na wazushi tokea siku nyingi tu. Eti NN mdingi ahahahahahaaaa.....usilolijua kweli lasumbua.

NN huyu kiukweli ni mkubwa kwangu.................... sema tu si unajua wanawake?? Mimba ya kwanza tu basi unakuwa ajuza....Believe me huyu anastahiki heshma yangu kama wewe naamini (Ila siku nikigundua u mdogo utaniamkia hadi niseme basi)
 


Nyie watu wawili.....naogopa kufanya name calling hapa kwa kuwa nawajua majina yenu halisi na profesheni zenu.......
Kuna tangazo la kazi pale chuo cha Ustawi wa jamii..........wanahitaji wahadhiri waandamizi..............you are damn good counselors asee!

MwanajamiiOne.....hebu chukua fomu asee...........nakushauri uanze na Certificate, haya mamjamaa yatakupasua kichwa ukianza na digrii!
 
Babu nawe umeona eh.........yaani nadhani muda wote wa skuli nitahakikisha naopt masomo yao...............
 

Wapo wanaofanikiwa kuwafanya watu wengine kuwapenda, kwa hili kama umependa haifai kukata tamaa.
 
Wapo wanaofanikiwa kuwafanya watu wengine kuwapenda, kwa hili kama umependa haifai kukata tamaa.

Huko ndo kunaitwa kujidanganya!!!
Utamfanya mtu akupende kwa lazima???Hilo haliwezekani!!Kinachotokeaga ni kwamba mtu anaamua ngoja tu niwe nae....siku akikutana na atakaempenda yeye bila ushawishi ndo unashangaa unaachwa kama vili hukuwahi kuwepo!
 
embu nikuulize Lizzy kwanini in the first place unaamua kuwa na mtu ukijua humpendi?



Huko ndo kunaitwa kujidanganya!!!
Utamfanya mtu akupende kwa lazima???Hilo haliwezekani!!Kinachotokeaga ni kwamba mtu anaamua ngoja tu niwe nae....siku akikutana na atakaempenda yeye bila ushawishi ndo unashangaa unaachwa kama vili hukuwahi kuwepo!
 
Wapo wanaofanikiwa kuwafanya watu wengine kuwapenda, kwa hili kama umependa haifai kukata tamaa.
Mkuu kuna kitu kinaitwa chemistry

kuipata hiyo ni kazi, ila ukiipata basi na kuipoteza ni kazi mara dufu

Love kama love iko very rare, but partnership and relationships are evrywhere, and our challenge is that "WE FAIL TO DIFFERENTIATE LOVE AND OTHER THINGS SIMILAR TO LOVE"

Wewe hujawahi kuona unakuwa na rafiki na unakua excited lakini baada ya mwezi tu unagundua jamaa wala hamuendani kwa chochote zaidi ya majasho tu?
 
sasa hapo pa kufall fro wrong types......Uwilll so we have types eh?? I thought mapenzi hayachagui na ukipenda unapenda?? Hebu tufundishane jamani kuidentify our types....tunapaswa kuangalia vitu gani??

MJ sure mapenzi hayachagui ila watu ndo wanaotakiwa kuchagua.

Hapa tuachane na yale ya ''love at first sight'' maana hiyo haitokei sana.Mara nyingi unapata nafasi ya kumjua mtu kidogo kabla yakuanza kumdondokea.Tatizo ni kwamba unaweza ukajua unachoangalia wewe (mf. maturity level....kama ni mtu anaetaka commitment...mtu mwenye malengo....responsible and so so) mwanzoni ukaonyeshwa hayo yote uliyotaka wewe kuyaona ila baada ya kudondoka ndo unaonyeshwa sio. Hapa kwakweli huwezi kusema tatizo lilikua wewe maana sio kwamba uliona mabaya ukajifanya kichwa ngumu ila umedanganywa tu.Sasa inapotokea hali kama hiyo umeshagundua kwamba Mr. Right is infact Mr. Wrong kosa lingine ambalo hua linafanyika ni kufikiria na kuamini kwamba anaweza kubadilika. Sio dozi ya mapenzi wala kujali inayoweza kumbadilisha mtu asiyetaka kubadilika.

Kwa wale wanaoona kwanzia mwanzo kwamba wamekosea njia ila bado wanajiaminisha kwamba labda tukiwa kwenye level nyingine atakua vile nitakavyo!Labda nikimuonyesha nampenda na yeye atanipenda.Labda nikimuonyesha mapenzi sana atajikuta nae ananipenda......Lots of labdaz bila muelekeo naweza kusema ni ujinga kwa kiasi flani....matendo yanasema mengi.Inabidi watu tujifunze kukubali kwamba kisichokuwepo hakipo tu.Na utakapokubali mapema kwamba hapa nimeshindwa the better.

Kitu kingine ambacho hua tunakosea sana ni kusoma mengi kwenye kitu kidogo.Unakuta mwenzako anachukulia uhusiano wenu kama kitu cha kusogeza muda tu wewe kwenye mawazo yako ndo umefika na unaamini kwamba nae amefika .We have to learn how to take things slow and hold back untill we know for sure where the whole thing is heading.

Back to the types.....kuna thread alinzishaga my dearest Michelle kuhusu wanaume ambao ukishawagundua ni vizuri kufunga moyo wako na kufuli na ukimbie bila kuangalia nyuma.

https://www.jamiiforums.com/mahusia...zangu-tuwe-makini-na-aina-hii-ya-wanaume.html
https://www.jamiiforums.com/mahusia...usiwe-kinganganizi-soma-alama-za-nyakati.html
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/115345-i-was-lonely-and-you-were-there.html
Angalia hizo thread.....might be helpful!
 
embu nikuulize Lizzy kwanini in the first place unaamua kuwa na mtu ukijua humpendi?

Hilo swali kwakweli siwezi kuwajibia wahusika maana wana sababu nyingi. Binafsi sijawahi kujidanganya ntampenda huko mbeleni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…