Inakuwaje Mambo haya??

Wapo wanaofanikiwa kuwafanya watu wengine kuwapenda, kwa hili kama umependa haifai kukata tamaa.

KAtavi ni kweli kabisa kuwa wapo wanaofanikiwa kuwarudisha waliotoka kwenye mstari wa mapenzi lakini ukichunguza sana utakuta kuwa kuna mawili
1. Aliyetoka (akarejeshwa) alikuwa na kajichembe ka penzi kwa huyu wa awali. Yaani pamoja na kutoka na kuwa na mwingine but naye alikuwa bado anampenda mwenzie basi tu alitaka kuonja ladha tofauti,
2. Inawezekana huko alikokwenda hapakuwa kiviiiile so anaona bora arudi kwa zimwi limjualo.......BUT wa aina hii mara nyingi kurudi kwao huwa ni kwa muda. Kwa kuwa hajapenda kiukweli basi atatuliza mzuka kidogo huku akiyatafuta makazi mengine .......so huyu anayehangaika kumrudisha mwenzie mstarini atakuwa anaumia tu.
 

nyamayao nlikuwa nakusubiri kweli kwenye hii thread..........dada haya mambo bwana. Asa usifikiri tunatendwa sie tu wanawake. Kuna wanaume wanatendwa hadi najiulizaga hivi huyu kwa mwanamke mwingine haiwezi??!! Kusema ukweli mapenzi ni noma. Kuna mkaka mmoja huyo yaani kwa miaka kadhaa sasa kashindwa hata kuoa kisa mwanamke ampendae kamtumikia na bado kasepa....so kaweka nadhiri haoi ah.....................................
 
hili lilinitokea mie, nilipenda nicpopendwa, niliachwa njia panda bila kujijua, swali la kujiuliza ni kwamba unakubali matokeo lakini huyo huyo kwassa ndio msumbufu na lawma kibao lakini yeye ndio alikutosa, maisha haya...

Hapo sasa nyamayao yaani kuacha aache yeye tena kwa mbwembwe afu aje alalamike ah............. na kuna kina dada nao tunafanya hivi ah ............
 
Na kwa nini ung'ang'anie kupenda mahali ambapo hupendeki? Tafuta akupendaye umpende!!

tripojo........laiti ingekuwa rahisi hivi kutambua na kukubali kuwa hapa sipo. Jamani acheni nadhani hayajawakuta.......mie I was like a zombie.....ukizingatia ndo alonifunza yaani nlimwona kama ndiye yeye peke yake lol..........Nakumbuka siku niko kwake nimemfulia, nikapika namaliza kutenga mezani ananiambia ........sasa mydia inabidi uondokke maana flan anakuja na nisingependa akukute hapa loh......nlijuta but thanx GOD that was the day I found my senses................ yaani nimpikie mwanamke mwenzangu nimtengee mezani yaani eh.....acheni jamani.

Ingawa alichomtendewa na yule mwanamke hakikuwa cha kiungwana but nilifurah kimoyomoyo........afu alitendwa kisha akakimbilia kwangu mie ambaye moyo ulishapata kutu....masikini.
 

Ha ha ha, mwj ...una visa wewe...mapenzi kimulimuli!
 
Ha ha ha, mwj ...una visa wewe...mapenzi kimulimuli!

Kaka Mbu we acha tu...mapenzi acheni jamani yaendeshe watu............... nakwambia mwanaume amesubiri miaka kumi na ushee.............binti kamwonyesha kila dalili kuwa mh hapana am not into you lakini wapi.........anakubali anampa space mdada anaendelea na maisha BUT Mkaka anafuatilia...mdada akitendwa tu mkaka vuuup huyo to give the shoulder to cry on...........yaani hadi sasa. Huwa natamanigi kweli kumwuliza kama kwa mwanamke mwingine haiwezi?? Nashindwa tu kwa kuwa namheshimu.........
 
Reactions: Mbu


...halafu kuna wataotumia short cuts Oooh, "kalishwa limbwata!...." hamna Limbwata wala nini,
jamaa kapenda tu. Ana matumaini na Imani hamna mkamilifu duniani.

Kuna kipindi mwenza wako ana cheat, ukishambamba...anajitetea akilia "haki ya nani sijui nilikumbwa na nini, kwanza wala siku enjoy lolote. Mawazo yangu yote yalikuwa kwako!" ...mwanaume unalegeza kidevu, kesi imeisha. Baada ya miezi miwili mitatu anarudia tena, halafu anajitetea kwa nyimbo hiyo hiyo.
Circus kwa kwenda mbele.
 
...halafu nyie? mnajua bila malaria, ...Klorokwini na Aspirin haziuziki!

Ndio maana tunapinga hizi dawa za kuua wadudu kama mbu....mbu wakiisha, klorokwini na aspirin tutakosa soko.

Mbu na aendelee kuwepo daima.

Fellow tablet na mosquito nigongeeni senksi hapa kabla sijaidiliti hii yuziful post........

Mjuu mtiifu sorry kwa hii yuzifuli ofu topiki..........gonga senksi kuonyesha ishara ya upendo.
 

kwa kupenda senksi tu hujambo haya senksi

The Following 2 Users Say Thank You to Asprin For This Useful Post:

Maty (Today), MwanajamiiOne (Today)​
 

ni mtu yackukute tu coz hujitambui kabisa kabisa, huyu wako alikuwa anakulazimisha uukubali mseto, unapika mwenzio anakuja kula, unafua mwenzio anakuja kulalia...nashukuru sana ulivyojichomoa huko, hii ilikuwa gunia ya msumari, kaka muwazi san huyo hataki matata...hiki kipande kimeniacha hoi bin taaban.

""sasa mydia inabidi uondokke maana flan anakuja na nisingependa akukute hapa loh.""
 
nyamayao we acha huyu kwa kweli hata simchukii tena maana naona kabisa amekuwa mwalimu wangu mzuri...yaani siku hizi nikimkumbuka ninaachia tabasamu pana utafkiri niko kwenye maonyesho ya mwanya!! ah...tena alikuwa anataja kabisa jina na huyo mdada mie nlikuwa namjua loh..........nlikuwa nkitaka kuwa naye nafanya booking mapema....na bado siwi na uhakika kwani siku ikifika atakwambia Flan kantuma nikamchukulie lunch box sijui wapi loh .....................mbavu sina leo
 
MJI usisahau msemo wa kutenda wema uende zako,huwaga hatuchelewi kulipwa ni hapa hapa na huwa haichukui mda mrefu.


 
MJI usisahau msemo wa kutenda wema uende zako,huwaga hatuchelewi kulipwa ni hapa hapa na huwa haichukui mda mrefu.
Kweli kabisa chauro.......nami nimejifunza.

I wish.......................... I wish ningejua unachowish hapo kwenye signature yako Mamito
 
Kwakweli mambo yamapenzi ni magumu sana pindi yanapokufika muda mwingine inabidi uchukuwe uamuzi ambao utaamuia kwa muda na kusahau kuliko kuwa mtumwa wa mapenzi mana kung'ang'ania sehemu usiyopendwa ni utumwa wa mapenzi,HUWEZI KUKUMBATIA JIKO JAPO LINAKUIVISHIA CHAKULA LAZIMA UTAUNGUA TU MAMA
 
Mumy maisha yana safari ndefu ................:tape:lakini yaache yalivo tu mpenzi karibu ndoto zangu zinatimia nitatoa na hako kasignature mwanzo nilifikiri hayawezekani,kumbe kwake yeye yote yanawezekana.


Kweli kabisa chauro.......nami nimejifunza.

I wish.......................... I wish ningejua unachowish hapo kwenye signature yako Mamito
 

hahaha huyu alikuwa kichwa maji wallaahh, khaa ssa MJ1 huyo mdada nae alikuwa anajua kama jamaa ana wewe?..kweli hapo ilibidi tu ulivue pendo kabisa, mtu kama huyu sasa hivi ukikutana nae unajiuliza mara mia mia kwann uliruhusu roho yako kuvunjika wakati ule, mie langu leo nimekuta mail yake eti linataka nimpe nafac ya kuongea nae Easter nikienda njoro, yaani me niache kunywa mbege nikaongee na zilipendwa tena nikaongee utumbo, madai yake yupo tayari kufanya lolote ili anirudishe kwenye himaya yake...mama wa watoto wawili aitelekeze familia yake kwa ajili ya huu upupu.....ovyo la mwisho.
 
 
halafu una hasira nyamayao,unawekaje hasira mda mrefu ivo watu kama hao usiwawekee hasira ni kuwatazama tu wakatafakari huko mbele ya safari.Hujawasikia na wale wanakuambia hawa watoto wangekuwa wa kwangu unabaki kucheka tu,na mashetani yake yakimtuma simu kwa kwenda mbele na marafiki zake kuja kukueleza upuuzi.

 

Hata sidhani kama yule alikuwa anaambiwa nlikuwa naambiwa mie ............nahisi mtima wa bwana ulikuwa zaidi kwa yule mie kwke alinichukulia mapozeo tu sikulijua hilo kuna siku tulikuwa wote barabarani tukapishana na huyo bi dada naye kapakizwa garini sijui na mnani basi wee.....nlijionea maajabu.... mkaka alitamani kuingiza gari chini ya uvungu wa lorry. Kumwuliza anajibaraguza nkamshushia vipande vyake ..........afu anabisha eti kwenye lile gari alokuwa anaendesha ni mwanamke loh.............mwishoni alikujaletewa mimba ya Mzimbabwe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…