Mjukuu mtiifu, babu ako haelewi maana ya hiyo hapo kwa red (damn uzee)...waweza kunidadavulia wakati naendelea kuielewa hii thread yako? Ahsante kwa kunielewa.
Wakati naendelea kuielewa, ngoja nikunong'oneze (Samahani sijapiga mswaki)......unajua kuwa mapenzi ni upofu na ukiziwi kwa apendaye pale asipopendwa?...atafanyiwa kila visa lakini atakuwa haoni, ataambiwa kila uchafu lakini atakuwa hasikii......
Sasa hii ya kurudi mara ya pili, baada ya wewe kumtapika, ukweli ni kuwa wakati ulivyokuwa ukimpenda ulikuwa unampa vitu vyote (ili usimpoteze, siyo?) Kama ni kitandani ulikuwa unawajibika ipasavyo, kama kiuchumi ulikuwa unamkabidhi kipato chako ili atumie atakavyo....... Kwa kifupi ulikuwa unampa kila kitu kwa gharama ya juu ili usimpoteze......Sasa huko aliko hapatiwi vitu hivyo, au alikuwa anapatiwa na sasa amenyimwa ghafla wakati bado ana kiu navyo.......... atapiga mahesabu yake na kuku-kumbuka "mjinga wake"......Atatafuta njia zote akurudie, atajifanya anajutia mabaya aliyokutendea, atamsingizia shetani, ataapa kwa miungu ya kwao kuwa hatakuumiza tena.........
Mjukuu mtiifu, amini, amini nakuambia.... Akirudi huyo usijidanganye, ukampa kama zamani, kiu yake ikikatika atakupiga pigo jingine kuu. Na mara nyingi pigo la pili laweza kuleta maafa makubwa zaidi.........usithubutu kukutwa, watakucheka watu!
Narudi kitandani kumalizia usingizi wakati nikiendelea kuielewa hii sredi.