Inakuwaje mashujaa hawa walioinusuru TANU hawajaadhimishwa hadi leo?

Kitabu hiki nakipataje make ukienda bookshops vitabu vya hivi havipatikani!! Naomba kujua nakipataje hadi kunifikia nilipo bukoba, means naomba kujua gharama zote
WilboardG,
Kitabu cha Abdul Sykes Kiswahili na Kiingereza vinapatikana
Ibn Hazm Media Centre, Msikiti wa Mtoro na Manyema na pia
Tanzania Publishing House (TPH) Dar es Salaam.

Ibn Hazm wanakiuza kwa shs: 10,000.00.
TPH wanakiuza kwa shs: 15,000.00
 
Samahani ndugu, mbona vitabu vya hivi hatuwezagi kuvikuta bookshops zaidi ya kukuta vya nyambari?? Nielekeze pa kukipata ikibidi niambiwe na gharama za kukifikisha Bukoba make ndo nyumbani
kitabu kinapatikana ilala Amana karibu BOA BANK
 
Mohamed Said,
Mimi sipo dar labda ningepewa utaratibu wa namna ya kukipata huku mikoani
 
WilbroadG,
Bahati mbaya mimi ni mwandishi maduka ya vitabu ndiyo wanaouza ikiwa watapenda.
 
Waislamu kwenye siasa wanaleta dini, kwenye elimu dini, kila kitu udini. Siku gani mtaweka dini pembeni mjadili mambo bila kuwaingiza wazee wenu waislamu ambao hawakuleta uhuru zaidi ya kumsomea mkoloni albadir? Usomi wa Nyerere ndiyo ulitupatia uhuru na hiyo ni fact! Waislamu wa Tanganyika at the time walikuwa hawana shule zaidi ya elimu ya madras.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shujaa Julius Nyerere tu! Wengine wenye vibandiko wasoma albadir tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia iliyofichwa
Historia inaandikwa au haiandikwi? Kama hao mashijaa wenu wangekuwa na elimu ya maana, na siyo ya madras basi wangeandika. Hakuna aliyeficha historia, nyinyi waislamu ni wachochezi sana. Kwani hiyo historia yenu Ilifichwa wapi na Nyerere?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WilboardG,
Kitabu cha Abdul Sykes Kiswahili na Kiingereza vinapatikana
Ibn Hazm Media Centre, Msikiti wa Mtoro na Manyema na pia
Tanzania Publishing House (TPH) Dar es Salaam.

Ibn Hazm wanakiuza kwa shs: 10,000.00.
TPH wanakiuza kwa shs: 15,000.00
Vitabu vya chokochoko tu hivyo! Unamjua Abdul Sykes wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shujaa Julius Nyerere tu! Wengine wenye vibandiko wasoma albadir tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mberoya,
Mbona ndugu yangu umeghadhibika kiasi hicho na hapa tuko katika
mjadala tu hatugombani?

Umesema kweli na umempa Baba wa Taifa haki na heshima stahiki
yake.

Lakini peke yake bila ya kupokelewa na wenye mji Baba wa Taifa
angeshindwa.

Unakijua kisa cha Rashid Ali Meli?

Unakijua kisa cha Idd Faiz Mafungo?
Unamjua Sheikh Mohamed Ramiyya?


Wa Kwanza Kushoto ni Idd Faiz Mafongo Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika wa Mwekahazina wa TANU. Wanaofuatia ni: Sheikh Mohamed Ramiya wa Bagamoyo, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu. Picha Hii ilipigwa Dodoma Railway Station Mwaka 1956 Wakati wa Kueneza TANU Katika Majimbo.

Unamjua Bi. Shariffa Bint Mzee?
Kukutajia majina machache.

Unajua historia za wazalendo hawa katika kupigania uhuru wa
Tanganyika?

Unajua hata historia ya Baba wa Taifa haiwezi kukamilika wala
kunoga bila ya kutaja michango ya wazalendo hawa?

Je unalijua Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh
Suleiman Takadir
(1954 - 1958) kisha Idd Tulio (1958 - 1963)?

Baraza lenyewe ndilo hilo hao chini:



Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Mohamed Said: KUTOKA JF: ALI MWINYI TAMBWE, RASHID ALI MELI NA IDD FAIZ MAFUNGO - SAFARI YA NYERERE UNO 1955
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…