Inakuwaje Mkurugenzi wa TBC mpaka sasa yupo kazini?

Inakuwaje Mkurugenzi wa TBC mpaka sasa yupo kazini?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Jana Waziri Mkuu Feki anatoka anatoa takwimu za uharibifu wa mali uliofanyika kipindi cha uchaguzi.

Ametaja magari ya serikali, magari binafsi, vituo vya polisi, nk. Tuache kwanza hoja ya usahihi wa hizo takwimu ambazo zinatia shaka.

Cha kushangaza wakati yote hayo yanatokea, kituo cha taifa ya Television TBC hakikuwa kinatoa taarifa yoyote wakati uharibifu huo unafanyika. Bado Mkurugenzi wa TBC, Ayub Rioba yupo ofisini anaendelea na kazi.

Jana wahariri wa vyombo vya habari wameitwa na serikali ili kidogo wasafishwe na warudishiwe imani yao kwa jamii. Wahariri wanalalamika kuwa wanaonekana wa hovyo mbele ya jamii na wanailalamikia serikali kwa kubanwa na kutishwa katika utendaji wao wa kazi. Je, kuna lolote wamejifunza?

Sasa hivi kuna hati ya mashitaka dhidi ya serikali ya Tanzania na viongozi wake kuhusiana na utekaji, mauaji na upotevu wa watu. Hati hii imewasilishwa huko ICC. Je, ni chombo gani cha habari cha ndani kimeripoti taarifa hiyo?

Narudia tena, kuna lolote wamejifunza?
 
Back
Top Bottom