Inakuwaje mtu mzima kukubali kuitwa chawa, kondoo?

Inakuwaje mtu mzima kukubali kuitwa chawa, kondoo?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Baada ya kukoloniwa na kutumikishwa, tuligeuzwa mazwazwa wasiotaka kusikia neno mabadiliko au ukombozi. Huwa inaniwia vigumu kwa mtu mzima tena mwingine msomi kukubali kuitwa chawa, kondoo au maamuma kana kwamba hawezi kujielimisha na kujikomboa akaukataa uchawa, ukondoo, na umamaamuma.

Tunachukiana, kuibianaa, kuhadaana hata kuuana tukigombea uchawa, ukondoo, ukuku, umaamuma na matusi mengine lukuki. Je inakuwaje mtu mzima na akili zake anajirahisi na kurahisishwa kiasi cha kuitwa matusi ndiyo aliwe au ashibe?
 
Back
Top Bottom