Inakuwaje nikimfikiria mtu ambaye sijamuona muda mrefu, nikija kumuulizia kwa watu ninaambiwa kafariki

Inakuwaje nikimfikiria mtu ambaye sijamuona muda mrefu, nikija kumuulizia kwa watu ninaambiwa kafariki

Hata Mimi nikimkumbuka sana mtu ambaye tulionana kitambo nikimuumizia naambiwa amefariki. Kuna wengine nikikutana tu na mtu anayefanana nae nikiulizia naambiwa amefariki
 
Hata Mimi nikimkumbuka sana mtu ambaye tulionana kitambo nikimuumizia naambiwa amefariki. Kuna wengine nikikutana tu na mtu anayefanana nae nikiulizia naambiwa amefariki
ni nini hii?? ina maana gani?? hakuna kitu kinaniumiza kama kujua mtu ninayemfaham kwa namna yoyote ile amefariki napata gagaziko
 
ni nini hii?? ina maana gani?? hakuna kitu kinaniumiza kama kujua mtu ninayemfaham kwa namna yoyote ile amefariki napata gagaziko
Mm pia sielewi kabisa yaani Kuna siku nikikutana na mtu anafanana sana na rafiki yangu ikabidi niulizie watu hivi mtu fulan yupo kwel nikaambiwa amefariki atazikwa siku flan niliumia sana yan
 
Mm pia sielewi kabisa yaani Kuna siku nikikutana na mtu anafanana sana na rafiki yangu ikabidi niulizie watu hivi mtu fulan yupo kwel nikaambiwa amefariki atazikwa siku flan niliumia sana yan
aisee ngoja tuendelee kunywa supu nyama tutazikuta chini tuendelee kusubiria
 
Habari za wakati huu,

Naombeni kujuzwa hii hua ina maana gani, yani ninakua namfikiria mtu ambae sjamuona muda mrefu mno ajabu nikikutana na mtu ninaejua anajua alipo nikimuulizia tu jibu no moja AMEFARIKI

Mara ya kwanza kunitokea, kuna classmates wenzangu nilikua nikielewana nao mno, sasa baada ya shule kila mtu kwenda kivyake baada ya mitandao kama facebook na instagram kuwepo nilijitahidi sana kuwatafuta sasa siku moja huko insta nikakutana na classmate wangu mwengine katika harakati za kuwaulizia hao wengine akanambia mmojawapo alifariki alikua anaumwa mwengine alifariki na uzazi ilinitesa mana nilikua hata nikiwa busy walikua hawatoki akilini mwangu

Nyingine nayo kuna kaka mmoja wakati nafanya kazi tulikua tunafanya kazi kwenye jengo moja ofisi tofauti,alitokea kunichunuku mno hata ikatokea mimi nikaacha kaz hapo nikaendelea na mambo yangu, ila sasa nikawa namfikiria mno kwamba sina namba na muda wa kwenda ofisini kwake sina nikawa najiambia nafsini nitaenda nikamsalimie yan nikawa kama nafsi inataka kwenda lakini mimi sjui uzito ulitokea wapi, sasa siku moja kuna mama ambaye tulikua wote kwenye hilo jengo akanipigia tukasalimiana akaniambia unamkumbuka Daud nikamjib yeah namkumbuka sana nimekua mzito kwenda kumsalimia tangu niondoke akanijibu amefariki tangu mwezi uloisha tena ukimuona mtu kama yeye njiani ukimbie kafariki ghafla na tulishamzika aisee skua sawa had leo najiuliza kuna nini?? kwa nini nikimfikiria mtu kama hivyo nakuja kuambiwa amefariki

Je, kuna meseji yoyote natakiwa kuijua na mimi kutokana na ufaham wangu wa nafsi sjui chochote?? naombeni kujuzwa kwa mwenye kujua

Mshana Jr Pascal Mayalla
Dah nina mada yake ngoja niitafute nikiikosa nitarudi na maelezo
 
Back
Top Bottom