Inakuwaje penzi lililochuja huku mmoja akiwa king'ang'anizi wakati amesababisha?

malamia

Member
Joined
Aug 18, 2011
Posts
50
Reaction score
14
Asalaam, kuna mshkaji ana dem wake wameishi takribani miaka 3 na wamebahatika kupata mtoto. Kutokana na maelezo ya mshkaji ni kwamba dem ndio alipenda kuzaa wakati mchizi bado hajaamua, basi msela akacheka na nyavu Kid huyo.

sasa dem baada ya kujifungua mpaka sasa amebadilika kitabia amekuwa kiburi, mtata, mbabe, akidai ashazaa na mchizi hivyo hawezi chomoa vinginevyo atamshikisha adabu ukizingatia vyombo vya sheria vipo sijui ustawi n.k sasa msela kaamua kujiengua dem anadai atajiua na msela ajiandae kutoa maelezo police na mambo mengine kibao. Ila ki kiukweli msela anasema hawezi tena kuishi na huyu dem mwenyewe anamwita nyapu.

Msela yuko radhi kuanza maisha upya ili nyapu achukue kila kilichopo ndani akaanze maisha na mtoto, lakini bado nyapu anadinda anadai hawezi kumwacha! sasa wandugu hapa inakuwaje? msela yuko njia panda japo ameshafanya maamuzi ila anaona kama misala inanukia nukia mbeleni huko, USHAURI PLEASE.

DAH HAYA MAHUSIANO WENGINE MWISHOWE TUNAOGOPA SASA
 
Huyo rafiki yako ni mshamba saana.hajui mapenzi wala nini? Huyo nyapu wake kaanza kiburi na ubabe kwa sababu gani? Yeye ndo anamchanganya maybe dada wa watu kachanganyikiwa maskini kaloose control.mwambie akae chini na nyapu wake maisha ni haya haya wamlee mtoto.ila kiukweli ameniboa.wanaume mungu tu awasamehe
 
"NYAPU" mmmhhh a haya bana .................................... ............................................. .......
 
Mwambie amchomolee kisema maana yeye ni msela.
 
wasichana mara nyingi ndio wa kwanza kulikoroga ukikubali kumwacha anaanza kukung'ang'ania
 
Mwambie amfikirie mtoto sasa maana ndio keshazaa tayari awe mtu mwenye majukumu, hayo ndio maisha ya mahusiano hapaswi kuyakimbia, anakabiliana nayo kigumugumu hivohivo
 
hizi lugha zingine,....mara nyapu..mara demu,......sasa huyo rafiki yako kama anamwita mpnz wake nyapu/demu huoni kama anakosea?....mwambie aache kumwita hayo majina ya kijeuri na kipuuzi na mpnz wake atamheshimu kama baba mtt wake
 
Mkuu hiyo lugha uliyotumia hata kama mtu kuchangia inakuwa issue ungemuita tuu mdada maana hayo maneno dem, nyapu msela, akadinda duh
 
wasichana mara nyingi ndio wa kwanza kulikoroga ukikubali kumwacha anaanza kukung'ang'ania

unajua kila mtu anakua na ndoto ya kuishi maisha na mtu wa aina fulani,..sasa tatizo linaloonekana kama ni ung'ang'anizi wa kina dada zetu pindi tunapowazalisha na kutaka kuwaaacha ni pale anapofikiri hataweza kumpata mwanaume wa ndoto yake akiwa na mtoto wa mwingine ,..another side of the coin_ni kwamba mwanaume hata kama una mtoto ni rahisi kumpata mwanamke wa ndoto zako......kwa hiyo si kwamba ni ving'ang'anizi kama tunavyofikiri ila wana sababu ya msingi kabisa.....if you think loud
 
Una-umri gani? It appears you are a junior member humu JF na ki-umri, maisha etc kama huyo rafikio na huyo dada. Wewe na huyo rafikio na huyo dada should wake up and get a life.....
 
Mpaka lugha inakera bana
badilisha hiyo lugha ndo watu watakuelewa na wachangie
 
Mwambie amfikirie mtoto sasa maana ndio keshazaa tayari awe mtu mwenye majukumu, hayo ndio maisha ya mahusiano hapaswi kuyakimbia, anakabiliana nayo kigumugumu hivohivo

Mtoto hata siku moja hawezi kuwa ndio solution ya matatizo ya kimahusiano...kung'ang'ania uhusiano m'bovu kwa sababu ya mtoto hujitendei haki...na wala humtendei haki mtoto. Ni bora mtoto akue katika mazingira ya single parent lakini ya amani, kuliko wazazi wote wawili lakini hakuna amani. I hate wanawake/wanaume wanaotumia watoto kama silaha ya mahusiano na kulipa kisasi au kutesa mwenza aliye achana naye!
 
Acha kudanganya umma na hiyo part 1 ya maelezo yako...
Isiwezekane kwasababu watoto ni ugonjwa ama?!Nawajua zaidi ya watu watano ambao wameolewa na wanaishi raha mstarehe na wanaume ambao sio waliozaa nao.Achilia mbali walio kwenye mahusiano tu...
 
Lizzy haina raha kuchangia jamaa katumia maneno mengi sana ya kuudhi
Na inawezekana ni yeye mwenyewe ndo maana akaiandika kivile
Wako ambao wamezaa na watu wengine na wakaolewa na wanaishi maisha mazuri tuu na wale watoto wanasomeshwa as if ni watoto wa familia moja
 
Mwenyewe nimechangia tu kupinga haya madai yasiyo na mshiko...watu wa aina hii ndo wanafanya wasichana wanaotoa mimba waongezeke.
 
Kwa maelezo yako wameishi miaka3 wamebahatika kupata mtoto1 huyo tayali ni mke nikosa kumpachika hayo majina imeonyesha yeye kakosa hekima naye ndomwenye kibul hujaweka makosa yahuyo bint sema vijana au wanaume wengi maisha ya kiwa mgum tunakimbilia kuacha mke akumbuke huyo kiumbe hana kosa mtoto atakosa malezi ya baba&mama
 
Mwenyewe nimechangia tu kupinga haya madai yasiyo na mshiko...watu wa aina hii ndo wanafanya wasichana wanaotoa mimba waongezeke.

yaani mtu anaanzisha topic tena inayohusu dada zake au mama zake ila anaandika maneno ya kule mtaani kwa vijana wa kijiweni na sijui anaetgemea hapa wote ni watu wa rika lake
 
mkuu,..unamaanisha mimi ndio huyu malamia au,......?...aaaaaaaaah! Acha hizo bana
 
mkuu,..unamaanisha mimi ndio huyu malamia au,......?...aaaaaaaaah! Acha hizo bana

Mkuu sio wewe bana
Nilikuwa namaanisha mtoa mada inawezekana ni yeye mwenyewe ndo maana kaja nayo hapa
 
Acha kudanganya umma na hiyo part 1 ya maelezo yako...
Isiwezekane kwasababu watoto ni ugonjwa ama?!Nawajua zaidi ya watu watano ambao wameolewa na wanaishi raha mstarehe na wanaume ambao sio waliozaa nao.Achilia mbali walio kwenye mahusiano tu...

umma upi?...kwani watu watano ndio tosha kujustfy huo mtazamo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…