Inakuwaje unaomba talaka halafu baada ya kuipata unaanza kuishi maisha yasiyo na mipaka?

Inakuwaje unaomba talaka halafu baada ya kuipata unaanza kuishi maisha yasiyo na mipaka?

Nimeona jambo hili kwa baadhi ya wanawake, hasa wale waliotoka kwenye ndoa Zenye changamoto.

Mwanamke anapokuwa kwenye ndoa yenye changamoto labda ameumizwa, amepuuzwa, amenyanyaswa au hakupata alichotarajia, anaweza kufikia uamuzi wa kuomba talaka. Hatua hii, kwa wengi, huonekana kama ujasiri na kujitambua.

Lakini kinachokuja baada ya hapo, ndicho kinachozua maswali.

Baada ya kutoka kwenye ndoa iliyokuwa inamtesa, badala ya kutulia na kujijenga upya, utaanza kuona mabadiliko makubwa ya kitabia. Mambo ambayo awali alikuwa anayasikia tu kwa wengine, sasa yanaanza kuonekana kwake.

Anaanza kuingia kwenye mahusiano mengi bila mwelekeo YAANI hakuna mipaka. Kama ana mtoto, mazingira ya mtoto pia yanabadilika kwakuwa anakutana na watu wengi tofauti kwenye maisha ya mama yake, jambo linaloweza kumchanganya na kumuathiri.

Mtu aliyekuwa na utaratibu na mipaka, anaanza kuishi maisha yasiyo na mpangilio, kurudi nyumbani usiku sana, ulevi kupita kiasi, na tabia nyingine za starehe bila kujali athari zake.

Kwa nje inaweza kuonekana kama anafurahia uhuru, lakini mara nyingi ndani yake kuna mchanganyiko wa maumivu, hasira, na hali ya kutafuta kujifariji au kusahau aliyopitia.

Kwanini uombe talaka ukaishi maisha ya hovyo?

Kuna wanawake wachache sana wanao survive BAADA ya talaka.

Mwanamke MMOJA aliomba talaKa akabadilika KUWA mlevi vibaya sana mpaka anapoteza fahamu na ANAWEZA kata mauno mbele ya wanae
umeongea kitu cha msingi sana, watu/wanandoa wengi uamini kuwa talaka ni jibu sahihi la changamoto zinazozipitia. Lakini baada ya kupeana talaka upande mmoja, au pande zote mbili ugundua kuwa walifanya maamuzi ya kijinga/yasiyo sahihi.

Mama mmoja alimlazimisha mme wake ampe talaka, mme wake alimkatalia mara nyingi akimwambia kuwa maamuzi anayoyafanya siyo sahihi.
Mwanamke akambuluza mmewe msahakamani, talaka ikatolewa wakagawana mali, kila mtu akaanza maisha yake.
Baada ya mwezi mmoja jamaa akaoa mke mwingine, mwanaume akaanza kushine, makunyanzi yakaondoka usoni.

Yule mwanamke mtalaka kuona hivyo akaanza visa kwa mwanaume hii ni baada ya kugundua kuwa alisukumwa na hisia na hasira kufanya maamuzi.

Kwa ujumla mtalaka huwa anapenda mwenzake aanza kuishi maisha ya kijehanamu, yenye dhiki, uchungu, na uzuni. Maisha yakiwa mazuri huwa wanaumia.
 
Talaka huwa haimuachi mwanandoa salama. Especially mke, lazima fuse ipasuke ubongoni.
Btw matatizo mengi yanayopelekea ndoa kuvunjika huwa yanaanzia rohoni. Ndiyo maana inashauriwa kwa wanandoa kuhudhuria semina na mafundisho ya ndoa mara kwa mara.
 
Mpaka anaomba hayo yaliyokuwa anaishi yalikuwa ya hovyo tayari...wanaume wa kiafrika mfumo dume umetuathiri sana ndomana ndoa zinavunjika
 
Back
Top Bottom