LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
We jamaa ni mwandishi mmoja mahiri sana humu na una expossure kubwa ila nashangaa unavyoandika kuhusu mambo haya ya mmomonyoko wa maadili kana kwamba hujui vyanzo vyake. Umegusia tabia ya usingo madha, hapo sawa. Ila fahamu huu mmonyoko umeanzia mbali na unachangiwa na mifumo na mitindo ya maisha ya kisasa. Mambo mengi ya kimaadili na miiko ya jamii zetu imeachwa. Harakati na siasa za kupinga mambo ya kimaadili yaliyoongoza jamii mbalimbali kutunza maadili yao zimepuuzwa mpaka zikaundiwa kampeni kuzitokomeza na kisha kuzitungia sheria kali. Huwezi ukabomoa misingi ya kulinda maadili ya jamii halafu ikibomoka mbeleni ukaanza kulialia maadili hayapo wakati yalishaondolewa na hayapo. Hili suala la single mother ni matokeo ya kuupuzia maadili ya jamii. Zamani ilikuwa ni mwiko na ni laana mbaya mwanamke kuishi bila mume, ilikuwa ni lazima apate mume, na kwa wanaume ni hivyo hivyo. Huwezi kuishi bila mke wakati huna matatizo mwilini na akilini. Ndoa ilikuwa ndio kielelezo cha maadili ya jamii na pia ni ibada