KERO Inamaana haya mashimo ya kwenye Barabara ya Kyela (Mbeya) mmegoma kuyafukia au mmeamua tu kuyapotezea?

KERO Inamaana haya mashimo ya kwenye Barabara ya Kyela (Mbeya) mmegoma kuyafukia au mmeamua tu kuyapotezea?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Hivi ni TANROADS inamaana haya mashimo kwenye hii Barabara ya Kyela kuelekea Junction hamuyaoni au ni ujeuri tu?

Hii Barabara imekuwa kero kubwa sana kwa sisi watumiaji maana ina mashimo Hadi basi, kila siku magari yana pasua vioo pamoja na kuvunja vipuri.

Kibaya zaidi naye Mbunge wetu anajifanya haioni hii kero au ndiyo anasubiri muda wa kampeni ufike aombee kura kwa kutoa ahadi za kurekebisha.

Ndugu Mbunge Ally Mlaghila Jumbe maarufu kama Kinanasi, hivi unazikumbuka zile ahadi zako kuhusu hii Barabara?

Serikali tunaomba mtusaidie kutatua hii kero maana soon tutaanza kushuhudia ajali.
DSC_0408.JPG

DSC_0407.JPG

DSC_0409.JPG

DSC_0412.JPG

DSC_0411.JPG

DSC_0419.JPG

DSC_0417.JPG

DSC_0413.JPG
 
Barabara ya kilwa, toka somanga, mpaka nangurukuru ni mashimo tu, maeneo yaliyoharibiwa na mvua za mwaka jana mpaka leo hayajakaa sawa, na mvua nyingine zinaanza muda si mrefu.

Nchi hii ni kama ina laana vile.
 
Nimecheka sababu wanapanga dili liweje, muda sahihi.

Maana nikiwa likizo jijini Dar, niliipita barabara moja maeneo ya ndugu zangu.. mwaka mzima walikuwa wanaziba viraka na ni vikubwaaaa haswa hata Makamu Waziri Mkuu wanapita daily ni eneo anaishi. Barabara ndefu ila wao ziba rudi ziba rudi na magari mkubwa mazito yanapita hapo sana.

Sielewi kwanini hawafanyi kazi za kudumu bali lami ya kudanganya ili warudie kazi kila mara.
 
Barabara ya kilwa, toka somanga, mpaka nangurukuru ni mashimo tu, maeneo yaliyoharibiwa na mvua za mwaka jana mpaka leo hayajakaa sawa, na mvua nyingine zinaanza muda si mrefu.

Nchi hii ni kama ina laana vile.
Hatari tupu
 
Back
Top Bottom