Inamaanisha nini kumheshimu BABA yako na MAMA Yako?

Inamaanisha nini kumheshimu BABA yako na MAMA Yako?

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Amri inayosema mheshimu baba yako na mama yako,inapatikana mara nyingi katika biblia.

(Kutoka 20:12, Kumbukumbu la Torati 5:16, Mathayo 15:4, Waefeso 6:2,3)


[ KUTII AMRI HIYO KUNAHUSISHA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:-]

1>-WATHAMINI:-Unawaheshimu baba
Na mama yako unaposhukuru kwa ajili ya mambo yote ambayo wamekufanyia,unaweza kuonyesha unawathamini kwa kutokudharau mwongozo wanaotoa juu ya maisha yako,mfano:-kama ndoa yako inamgogoro ufanye nini,inatakiwa ujivunie kuwa na wazazi wako,usiwatenge kwa marafiki zako,daima uwape kipaumbele cha kwanza kwa kitu chochote..

2>-KUBALI MAMLAKA YAO:-Hasa ukiwa wewe ni kijana,onyesha kwamba unawaheshimu baba na mama yako,unapotambua mamlaka ambayo mungu amewapa juu yako.

3>-WATENDEE KWA HESHIMA:-mara nyingi,hilo linahusisha jambo unalosema na jinsi unavyolisema.ni kweli kwamba nyakati fulani kuna wazazi ambao hutenda kwa njia ambayo ni ngumu kuwaheshimi.hata hivyo watoto wanaweza kuwaheshimu wazazi wao kwa kuepuka kuzungumza au kutenda kwa njia isiyo na heshima.

4>-WAPE MAHITAJI YAO :-wazazi wako wanapozeeka huenda wakahitaji kutuzwa,jitahidi kwa kadri uwezavyo kuhakikisha kwamba unawatunza wazazi wako

Yajayo yanafurahisha, one for the road.
 
Back
Top Bottom