Inamaanisha nini?

Eti uzungu uzungu hata ningekuwa mie Fidel ningemaka kwa sababu huyo dada sifa zake si haba sasa nikiona Mr kareact hivyo nikaekimya na kufungulia magonjwa mlango? Nyie wanaume sijui mkoje yaani mnatake kila kitu simple tu!!

Mmh M1 umenishtua!! hii sentensi huwa anapenda sana kuitamka my wife ... hivi ni kweli kwamba wanaume we are taking everything in its slightest weight?? me nahisi wakati mwingine wanawake huwa mnakuwa na presha za ajabu sana ... kitu kidogo tu mna wasiwasi kweli ... na sasa naamini huu upungufu wenu ndio unaopelekea wakati mwingine nyie kufanya maamuzi yasiyo ya busara!!

kuweni na confidence dada zangu!!
 
Ok nimekuelewa inawezekana ikawa hivyo but what if lilikuwa swali genuine tu la kawaida. Mimi nimekaa ofcn kwangu nikasikia mtu akiitwa flani anafanya kazi ofc ya mume wangu- sitakiwi kumwuliza mume wangu kama anamfahamu? mbaya zaidi huyo niliyemsikia ana ubini sawa na mume wangu pengine nataka kujua kama ni mmoja wa wifi zangu nisiyemjua?? Wajameni kwa nini kujishuku? au basi angeuliza kafanyaje? au ndio nani? lakini si mitusi aloshushiwa bi dada!!
 

Madabwada mie mkeo!! lol

Ni kweli pengine we are worrying over just everything!! Inatukost but huwa hatuworry unless tumehisi kitu Mr!
 

Muulize vizuri huyo rafiki yako. Pengine kuna kitu anaficha, hawezi kutukanwa tu na mumewe kisa kauliza kama mumewe anamfahamu mtu fulani wa ofisini kwao!
 
HAHAHAHAH..Sijacheka toka siku ianze... thanks for making my day!
hakuna cha sangoma wala nini!

Basi weka vitu hadharani mama! Ukienda PM na kajukuu kangu muda si mrefu kina bht, charity, nyamayao,pearl nk nk nk watakutafutia huko. Siku nzima itaishia uko kwenye PM afu wenye kiu na wewe tukafa na kiu yetu!
 
Basi weka vitu hadharani mama! Ukienda PM na kajukuu kangu muda si mrefu kina bht, charity, nyamayao,pearl nk nk nk watakutafutia huko. Siku nzima itaishia uko kwenye PM afu wenye kiu na wewe tukafa na kiu yetu!

siyo kila kesi inasikilizwa mahakama ya wazi...nyingine husikilizwa chamber - in camera- hakuna waandishi wa habari wala wasikilizaji.Ni kwa faida ya jamii lol!
 
siyo kila kesi inasikilizwa mahakama ya wazi...nyingine husikilizwa chamber - in camera- hakuna waandishi wa habari wala wasikilizaji.Ni kwa faida ya jamii lol!

Hehehe! Ngoja waifu akinitaka nikapime Ngoma ntaku-PM tutete! LOL!
 
Madabwada mie mkeo!! lol

Ni kweli pengine we are worrying over just everything!! Inatukost but huwa hatuworry unless tumehisi kitu Mr!

Hhahahaa ... inawezekana ni wife 🙂

i'll tell u a similar story .... home kwetu kuna mpangaji mmoja amehamia karibuni ... wife katika pitapita zake saloon akapata story za huyo dada kwamba ni kiwembe balaa .. yaani huwa hachagui .. waume za watu, makonda, vijana ... yeye twende kazi ... na bahati mbaya ni wa kutoka kule kwetu nanhiii (wajua tena) basi ndo wife akatia tick kabisa.

akaja akanipa hiyo ishu .. me nkamwambie aniondolee umbeya wake ... huwa si-judge mtu kwa maneno ya watu .. duuh .. ikawa kosa ... akatamka hiyo sentensi yako kuchukulia vitu simpo ... na kweli ... siku si nyingi yule mdada si akaanza kuniweka kwenye timing ... vimitego tego vya ajabu kibao (mara anivizie asubuhi nikiwa nakwenda job ananisimamisha na anachonieleza hata hakina mashiko; mara aniite dirishani kwake ... basi taabu tupu).... mmh nikaona sasa sooh ... ili kutunza heshima yangu na ya mke wangu ikabidi tu niwe nampa nyepesi kuhusu vituko vya huyo dada anavyo nifanyia ...

Eeh bwana wee ndo kama nilifanya kosa ... yaani wife ametokea kumchukia huyo dada mpaka balaa ... yaani hampendi hata kumwona ... kusalimiana hawasalimiani yaani ni chui na paka ... me ilibidi nimpige mkwara aacha hayo mambo yake ya ajabu coz me najua nifanyalo, nina akili zangu timamu na siwezi fanya huo upumbavu hata atumie nguvu zake za giza (coz yasadikika huwa anaenda kwa babu!!) na afterall adui yako inabidi umpende kwani kusalimiana kitu gani?? lkn nahisi juhudi zangu hazija zaa matunda, akanambia "we swetie kila kitu unakichulia kwa wepesi tu", .... nimeamua tu nimwache ... me huwa nasalimiana vizuri tu na huyo dada ila i always keep a distance from her coz ni kimeo kwa kweli ... hivi niongeapo wife anataka tuame kitaa though anatumia sababu nyingine ku-justify request yake but me nimeshaelewa ni kwanini ... nimemwambia hatuami n'go coz sehemu tulipo ni very strategic kwa makazi na biashara zetu ... basi nimemwacha kanuna tu!!

sasa najiuliza nimefanya kosa kuwa muwazi kwa mke wangu?? hii yaweza nishawishi nisimweleze mambo yanayofanana na hilo coz nahisi moyo wake ni mwepesi!!

so mamii MJ1 (my wife) tuaminini waume zenu jamani ... tuko care sana, tunawajali na tunawapenda sana! but mzidi kutuombea!! (poleni kwa bandiko lefu!!)


MDBD
 
Hapa mbinu au technics za uulizaji zilikuwa ZERO ukiwa na technics zero lazima upigwe bao. sio lazima awe huyo dada alishamvinjari, ila kama uulizaji ulikuwa ki wivu wivu wivu wivu mwanamme yeyote atachukia, Uanzaji wa swali eti unamjua.......haufai inaonyesha tayari anamtuhumu na kesha hukumu, nenda straight kwenye point,....fulani alikuwa anasema msichana fulani jirani na ofisini kwenu yupo hivi. Hapo hapo anasmsoma muewe alama za nyakati aone anaupokeaje ujumbe huo.Si ajabu angejibwa; ni kweli yule ni malaya au siyo au sijui.....Mwambie shogayo wanaume hawaulizwi wala kufumaniwa hivyo.Mweleze Inawezekana huyo mdada hana uhusiano naye alikosea kumuuliza.Endelea kueleza kuwa shem hawezi fanya hivyo. Siku zote usichekelee matatizo ya shogayo (sijasema umechekelea).Ndoa ni raha tupu mkitumia busara.
 
Hehehe! Tatizo yeye ndiye mshauri nasaha! Kama walikuja kanisani basi mama watoto huenda naye alikuja. Shirika lao ndo lina kampeni hiyo. Unaona maajabu haya? Waifu ni kansela lakini mume anaogopa kupima! Thanks God yeye huwa anapima. If she is OK, am OK! Thats my principle!
BTW na wewe ulipima au uliliacha hilo jukumu kwa watoto? Najua mzee hakupima, sina haja ya kukuuliza!
 


hahahahah... usichukulie kuwa kwa vile yeye kakutwa ok na wewe uko ok... ushasikia kuhusu discordant couples?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…