Inamaanisha nini?

Inamaanisha nini?

Ninadhani ndoa hiyo ina migogoro ya muda mrefu kiasi kwamba mume amekuwa sensitive sana na maswali ya jinsi hiyo. So ili kujilinda, inabidi aporomoshe matusi ili maswali yasiendelee.

Kuna polite way ya kuuliza maswali sensitive, inaonekana muulizaji hakutumia polite language. Mhusika akiulizwa swali kishari shari anaweza kujibu ama kwa mkato au akaporomosha matusi. Kwenye mahusiano/ndoa unapouliza maswali ya kishari/kipolisi au kama ya kitimoto, always huwa hayaishii pazuri. Mara nyingi huwa inaongeza tension hasa kama mahusiano/ndoa hiyo ina historia ya kutuhumiana/kutoaaminiana.

Nina refer majibu ya mhusika, "mimi si malaya/mhuni wa kutembea na KILA CHANGU". So inaonyesha alishatuhumiwa/fumaniwa/shikwa akitoka nje ya ndoa.

Kwa hiyo kuuliza maswali sensitive sometimes kunahitaji hekima ya kutosha, kuangalia mazingira na trend ya mahusiano/ndoa. Suppose watu wametoka kugombana asubuhi hiyo ama jana yake usiku mke alimnyima mume wake, au mume alichelewa kurudi nyumbani unategemea jamaa akikumbana na swali kama hilo hataacha kutoa matusi? Maana wengi wetu kabla ya kujibu maswali ya jinsi hiyo lazima huwa tunajiuliza, kwanini kaniuliza? Ndipo kwa haraka mtu anaweza kuunganisha dots ambazo zinaweza kuwa sahihi ama siyo sahihi, matokeo yake ni kuporomosha matusi ama majibu ya mkato.

Ni ngumu kumhukumu huyo mwanaume kama anammega huyo dada au la, kwa kuwa tu ameporomosha matusi. Kwa maoni yangu, ninahisi kuna mengine ya ziada ambayo wachangiaji na MJ1 hatuyajui. More details plz!

Keil umejibu vema nashukuru kwa mchango wako. Lakini nikuulize swali moja ina maana hakuna njia nyingine ya kistaarabu ambayo huyo mbaba angetumia kufikisha ujumbe wake zaidi ya matusi? Hamjui ndo mnatupa hint mnaporeact tunaamini kuna kitu?
 
It beats me!
Hivi kwenye ndoa huu ndio utaratibu wa kuonyesha kutoridhika, wa kukwepesha usiyotaka? Kwani ukijibu kistaarabu bila kutoa/kuporomosha matusi hutasikika?

Ndiyo maana nilisema inategemeana na trend ya ndoa yenyewe, na pia wahusika wenyewe jinsi wanavyowasiliana. Tatizo lililo kwenye ndoa nyingi ni kwamba communication skills ni zero. Pia mashindano, mwanaume/mwanamke akipata clue kuhusu nyendo za mke/gf/mume/bf huenda kwa papara/hamaki/jazba, kiasi kwamba badala ya kumsaidia kumrekebisha unakuta unazidi kumharibu. Matokeo yake ni matusi na sometimes ngumi kabisa.

Nadhani taasisi ya ndoa kwa siku hizi leaves much to be desired! Nadhani there is something fundamentally wrong somewhere kama wanandoa - baba na mama wenye dhamana ya kulea na kukuza kizazi kijacho wana tabia za namna hii.

Kuna wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajui ndoa ni nini na kwanini waliingia kwenye ndoa. Ama waliingia kwa mkumbo kwamba kwa kuwa fulani kaoa/kaolewa na mimi ngoja nioe/niolewe, na matokeo yake ni hayo.

Hivi heshima bado itakuwepo? Nashindwa kuelewa inakuwaje endapo mke naye atatumia defence mechanism ya matusi - ndoa zingesimama?
Samahani kuuliza maswali mengi badala ya majibu.

Jino kwa jino ... kwani hujawahi kuona mke na mume wanatukanana mtaani na wapita njia wanawaona? Hujawahi kuona wanandoa wanatukanana mbele za watoto wao ama mbele za wapangaji wengine?

Watu wakishaanza kutukanana hapo kitu kinaitwa heshima kinapotea moja kwa moja. Mtu unaemheshimu huwezi kumtukana. Huwezi kumwita mkeo/mumeo mjinga, malaya ama mpumbafu; ilikuwaje ukakubali kuoa ama kuolewa na mtu wa sifa hizo? Impliedly na wewe unayetukana hayo matusi nawe una sifa hizo chafu ambazo unamtukana nazo!
 
Nadhani there is something fundamentally wrong somewhere kama wanandoa - baba na mama wenye dhamana ya kulea na kukuza kizazi kijacho wana tabia za namna hii.

Hivi heshima bado itakuwepo? Nashindwa kuelewa inakuwaje endapo mke naye atatumia defence mechanism ya matusi - ndoa zingesimama?
Samahani kuuliza maswali mengi badala ya majibu.


Not only someTHING, it is Lotz 'n lotz of stuff! actually kuna haja ya kuaddress hii kitu kwenye forums; kuna gap kubwa ya elimu ya maisha na kwa kiasi kikubwa vijana wengi tunaingia kwenye ndoa half prepared! Inasemwa sana na itaendelea kusemwa ila tusipolishughulikia haya ni shemu ya matokeo yake!
 
Aksante Ben inawezekana ni wasiwasi tu but hii reaction ndo imeshangaza na mpaka sasa Mr hajajisikia kusema lolote juu ya hili ah amekaa kimya kama maji ya mtungini

But sasa hii inatia wasiwasi,the guy must be mercyless coz kama unampenda mpenzi wako halafu unajua ni kitu gani kinamkoseha raha still umekaa kimya tu?Angalao angechukua hatua ya kuongea na mke wakee amweleweshe.kutulia kwake sasa kunaonyesha kwamba anaona amefanikiwa kumkaripia na mambo yamekua shwari

Kwa kweli si vizuri.Hata kama sasa jamaa alikua na Mood swings zitakua zimeisha
 
Not only someTHING, it is Lotz 'n lotz of stuff! actually kuna haja ya kuaddress hii kitu kwenye forums; kuna gap kubwa ya elimu ya maisha na kwa kiasi kikubwa vijana wengi tunaingia kwenye ndoa half prepared! Inasemwa sana na itaendelea kusemwa ila tusipolishughulikia haya ni shemu ya matokeo yake!

unachesema MasJ, na alichosema Keil kwenye post yake ya mwisho nadhani kina ukweli mwingi mno.Wanandoa wengi wa "kizazi kipya" mostly wanahitaji people-skills- wajue namna ya kuishi watu wawili kwa ku accomodate na tolerate each other - wajue maneno gani watumie/wasitumie, wajue namna ya ku manage conflicts kwenye its full cycle - ( conflict starts kidogo kidogo... mara mtu kanuna, hasemi au anasema mkatomkato, huu siyo mwanzo bali ni dalili tu kuwa there is something wrong.Hadi wanaanza kuulizana na kujibishana ujue hapo ingekuwa nchi ndio vita imelipuka watu wanarusha ma RPG,SCUD etc.. kumbe wangeweza kukaa mezani wakaongea na kukubaliana!)
In short nadhani watanzania kwa sasa wanahitaji kuwa na forum ya wazi kuzungumzia namna ya mawasiliano ndani ya ndoa.... huko tunakoelekea ni kubaya.Kuna siku tutaanza kuona/kusikia yanayotokea ulaya - mke/mume kamchinja, kamuwekea sumu, kakodishia mwenzie contract killers...kacharanga na kuhifadhi vipande kwenye mifuko ya plastic na kuchimbia kwenye backyard! God forbid...ndoa zinaelekea kubaya.
 
Jamaa anajihami keshavinjari na huyo shosti nwenye miwaya,pia nikama vile kaichoka ndoa.Anaogopa kivuli chake
 
Keil umejibu vema nashukuru kwa mchango wako. Lakini nikuulize swali moja ina maana hakuna njia nyingine ya kistaarabu ambayo huyo mbaba angetumia kufikisha ujumbe wake zaidi ya matusi? Hamjui ndo mnatupa hint mnaporeact tunaamini kuna kitu?

Naomba niseme kwamba kwa mtu ambaye siyo mstaarab matusi, ukali na majibu ya mkato ni shortcut ya ku-hide uchafu wake.

Ningekuwa ni mimi nisingetoa matusi na esp kama ninajishuku, kwa kuwa nikitoa matusi ni sawa na kumwagia petroli kwenye moto ambao unawaka. Ningekuwa mpole, ili nikigundulika nina kosa niweze kuomba msamaha.

Matusi, majibu ya mkato na ukali huwa yana raise red flag na kuongeza suspicion. Kwanza hujui kakuuliza kwa ajili ya nini. Kama unajishuku, hujui ana ushahidi kiasi gani. Ukiwa mkali na akaja kukushukia na ushahidi usiokwepeka, sijui utaficha wapi uso wa aibu?

Lakini kuna watu wengine huwa hawana aibu, anakuwa mkali na matusi mazito. Ukija na ushahidi usiokwepeka bado atakomaa na mitusi yake na haombi msamaha. Sasa hapo ndipo ninaposema kwamba inabidi kuangalia trend ya mahusiano/ndoa.

Ukikutana na mtu ambaye maneno kama samahani, pole, au asante hayako kwenye misamiati yake, basi jifikirie mara 2 kabla hujaji-commit. Ni mtu gani ambaye asiyekosea kiasi kwamba asijue neno samahani? Ni mtu gani asiye na feelings kiasi kwamba hajui maumivu na kuumiza? Ni mtu gani asiyejua ku-appreciate hata kwa kitu kidogo?
 
Back
Top Bottom