Inanauma sana.kama ni wewe ungefanyaje?

Inanauma sana.kama ni wewe ungefanyaje?

LuCKNOVICH

Senior Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
104
Reaction score
11
Nimepita mahala nikakuta my carpet na wadada wengine wanapiga story,kilichoniuma zaidi ni kusikia mimi naitwa buzi.na aliyetamka hivyo ni wife.Je ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Hahahahaaaa wife wako anakuita ww buzi? Lakini si mara ya kwanza kusikia wake za watu wanawaita waume zao mabuzi. Misemo ya mtaani hii inatupeleka kubaya. Mimi nafikiri njia nzuri mvae na umwambie akueleze sababu ya yeye kukuita ww buzi. Ukimuacha utakuwa unafuga ugonjwa ambao hautatibika hapo baadae. Sijasema upigane, muulize kwa hekima tuu. NA kama ana akili sawasawa hatoludia kukuita ww buzi.
 
Wife anakuita buzi???? Hahahahahaha! Mwambie umemsikia akikuita buzi so akwambie kwa nini anakuita hvyo! Huyo wife mwangalie sana!
Nimepita mahala nikakuta my carpet na wadada wengine wanapiga story,kilichoniuma zaidi ni kusikia mimi naitwa buzi.na aliyetamka hivyo ni wife.Je ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
pole sana kaka...vumilia hiyo ndio ndoa yenyewe.....uvumilivu ni wa muhimu kaka...Mungu yupo atakupigania
 
Nimepita mahala nikakuta my carpet na wadada wengine wanapiga story,kilichoniuma zaidi ni kusikia mimi naitwa buzi.na aliyetamka hivyo ni wife.Je ungekuwa wewe ungefanyaje?

Acha uongo wako wewe. Vinginevyo si mkeo bali ni hawara. Sidhani kama kuna mwanamke aliye kwenye ndoa anaweza kumwita mumewe buzi. Hii ni fabricated story.
 
Wengi wapo kimasilahi, wakitimiza lengo na kuondoka- top C. Usikatae labda ni kweli kaitwa buzi.
Acha uongo wako wewe. Vinginevyo si mkeo bali ni hawara. Sidhani kama kuna mwanamke aliye kwenye ndoa anaweza kumwita mumewe buzi. Hii ni fabricated story.
 
mkishaanza kuripoti mambo yenu ya ndani hapa ni dalili za kuchokana huko...mkalishe kitako,malizeni mambo yenu ndani kwenu huko
 
hahahaaa pole kwa kuitwa mbuzi! ila kwa sababu we ni mume basi we utakua beberu ye atakua mrs beberu, au?
 
Hahahahaaaa wife wako anakuita ww buzi? Lakini si mara ya kwanza kusikia wake za watu wanawaita waume zao mabuzi. Misemo ya mtaani hii inatupeleka kubaya. Mimi nafikiri njia nzuri mvae na umwambie akueleze sababu ya yeye kukuita ww buzi. Ukimuacha utakuwa unafuga ugonjwa ambao hautatibika hapo baadae. Sijasema upigane, muulize kwa hekima tuu. NA kama ana akili sawasawa hatoludia kukuita ww buzi.
Thanks Wakumwitu
 
hahahaaa pole kwa kuitwa mbuzi! ila kwa sababu we ni mume basi we utakua beberu ye atakua mrs beberu, au?

nimeuliza kama ni ww ungefanyaje.to me i think ni bora kuitwa buzi kuliko beberu
 
Mwangalie vzuri huyo wife wako kama kweli kakuita buzi. Muulizd vizuri. Wanawake baadh wanafata mikumbo tu ya wanawake mashangingi. Asije kuwa anakufanya saccos au vikoba kwa malengo yake. Pole sana.
 
si vizuri kwa mke wa ndoa kumwita mumewe buzi...hii inaonyesha lack of respect,...haileti picha nzuri kabisa....ongea nae muulize....mwambie kuwa hukufurahishwa pale ulipomsikia akikuita buzi.....:nerd:
 
mi nilshasema siku nyingi, love died on the cross with jesus....kilichobaki hapa ni kuchunana tu. ila kwa mm, pesa ninazo akinichuna naona sawa.
 
Itakuwa vizuri ukimuuliza si ajabu ulisikia vibaya....Pia inawezekana ulichokisikia ndicho hicho alichotamka labda ukimuuliza maelezo atakayokupa yatakuridhisha na hivyo kuondoa wasiwasi/hasira za kuitwa BUZI na mkeo.
 
thanks Mkuu i will try hiyo
 
Acha uongo wako wewe. Vinginevyo si mkeo bali ni hawara. Sidhani kama kuna mwanamke aliye kwenye ndoa anaweza kumwita mumewe buzi. Hii ni fabricated story.
Mi naamini ni kweli....sababu nimeshawahi kukutana na mkasa unaofanana na huo....ndoa zina mambo,uhadithiwe tu ndugu yangu mazingira.
 
Mkuu kama ni kweli basi mwenzetu ahesabu kuwa hana mke bali kimada.
 
Mambo ya wanawake waachie wanawake. Ukiyafuatilia sana utaumiza kchwa bure
 
Mkuu
Unaonaje ukam-demote, naamini akiwa ex-anaweza akajitambua na kujirekebisha kama atabahatika tena kuonekana na mwanamume mwingine. Hiyo ni ishara kwamba yupo kimasahi zaidi. zinduka kaka
 
Kwani mkuu mmefunga ndoa? Kanisani au msikitini? Kama ndiyo kaa naye kiutu uzima na umweleze, huenda aliongea kunogesha jamvi.
Kama bado ila mnataraji basi kuwa makini naye sana, si ajabu ukawa unamlisha na mume mwenzio.
Pasaka njema!
 
Back
Top Bottom