Pole sana Mkuu. Japokuwa umeambiwa kuwa alikuwa anataka kukutoa kafara, lakini huna udhibitisho kama ni kweli. Inaonyesha kama alitaka kukuona tokea mapema lakini ndugu zako hawakumpa hiyo nafasi.
Definitely, utakuwa na mixed feelings za kumwona na hilo ni sawa kabisa hasa kutokana na uliyoambiwa. Hilo linaeleweka. Lakini usimhukumu kwa maneno ya kusikia. Kutana nae na msikilize anasema nini unless kama na wewe unaamini sana ushirikina. Then, from there unaweza kufanya maamuzi ya busara na hekima.
Lakini kama walivyoshauri wengine kutana nae kwenye mazingira yaliyo ya wazi na sehemu yenye watu. Ikiwezekana kutana nae in some sort of a meeting na ndugu wengine. Ukiona anasita then jua ana lake. Lakini akikubali msikilize. Hata watu walioua wanapewa haki ya kusikilizwa.
Ukiamua kutokutana nae kama bado ana nia mbaya, bado anaweza kukupata tuu. kwani alipataje namba ya simu yako? Kama ukienda tungependa sana kama utatupa feedback.
Mkuu, hizi sehemu nilizoziwacha zinahusika na maoni mabayo ningetoa.
Ezan Mkuu, angalia haya aliyoyasema EMT. Hapa umesikia hadithi ya upande mmoja tu toka kwa wazazi na jamaa zako, lakini hujui chochote toka upande mwengine. Lakini kwa maoni yangu, hadithi uliyopewa na jamaa zako inaficha ukweli wote. Hilo la kuwa alitaka kukutoa kafara inaonesha ni kauli ya chuki juu ya kile baba yako alifanya, kauli ambayo kama ukimwambia mtoto mdogo anaweza kuamini na kuogopa, lakini wewe ni mtu mzima, na sidhani kama unaamini ushirikina. Kama kweli baba yako alitaka kukutoa kafara, sioni kwa nini alishindwa na anashindwa mpaka leo kufanya hivyo. Kwa kuwa alipata nambari yako ya simu, uelewe kuwa anakujua hata unapokaa na nyendo zako zote. Usiogope Mkuu.
Unaweza kufanya yafuatayo:
- Kama unataka kulitatua kwa haraka, nenda kamwone na msikilize, bila ya uoga, wala kumweleza kile ambacho uliambiwa. Sioni mantiki ya kwa lazima uende kumwona mahali palipo na watu, isipokuwa kama huyo baba ni kichaa kweli kweli.
- Kama una wakati wa kufuatilia zaidi, rejea kijijini kwenu na kumwona huyo rafiki wa bibi yako, anaweza akawa na ukwli tafauti na ulioelezwa.
- Njia nyengine, muambie wazi kuwa mnataka mkutane kukiwa na wakuu wa dini au imani yako, iwe kanisani, msikititni au popote.
Mwisho, kama ilivyokwisha semwa, usiwache kumwona bado yupo hai. Kwa vyovyote, huyo ni baba yako.
Kila la heri.
-